Na Tegemeo Kastus
Uzinduzi wa uogeshaji wa mifugo Umefanyika kimkoa jana katika kijiji cha Endabash Tarafa ya Endabash. Zoezi lilihusisha wataalamu wa mifugo wa Mkoa wa Arusha sambamba na wataalamu wa mifugo wa Wilaya ya karatu. Mgeni rasmi katika ufunguzi wa zoezi hilo ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Mheshimiwa Theresia Mahongo.
Katika hotuba yake ya uzinduzi Mheshimiwa Theresia Mahongo amesema wilaya ina majosho 26 na majosho 3 ndio yanafanya kazi. Mkoa wa arusha una ng’ombe 1,859,404 wilaya ya karatu ina ng’ombe 166,157 ina mbuzi 258,729 ina kondoo 85,997 takwimu ni kutokana na zoezi la upigaji chapa mifugo. Mheshimiwa Theresia amepongeza wafugaji na wanakijiji wa Endabash kwa kukarabati josho la mnadani, amesema katika soko la mifugo ambalo lipo wilaya ya Longido Namanga mifugo mingi inayouzwa katika soko hilo inatoka wilaya ya Karatu. Ameomba wananchi wasipite njia za mkato kwenda kuuza mifugo ili serikali iweze kuongeza mapato.
Mheshimiwa Theresia Mahongo amesema katika kutekeleza ilani ya chama cha mapinduzi, serikali imetoa dawa kwa ajili ya kuogesha mifugo kwa majosho yote yanayofanya kazi. Mheshimiwa Theresia amesema Waziri Wa Mifugo Mheshimiwa Luhaga Mpina 7/12/2018 katika mkutano wa Madakatari wa mifugo uliofanyika nchi nzima Arusha aliagiza majosho yote yaliyo kwenye Halmashauri yanakarabatiwe. Mheshimiwa Theresia amesema serikali imetoa dawa ya kuanzia kuogesha mifugo hivyo kamati za majosho zikae zipange bei za uogeshaji mifugo ili kuweza kununua dawa, wakati wa kupanga bei ni vizuri kushirikisha wafugaji. Amesema ni marufuku kwa wafugaji kufika kwenye josho na kuosha kinyemela na kinyume na ratiba zitakavyopangwa.
Mheshimiwa Theresia amesema mifugo inatakiwa kuogesha mara mbili wakati wa kiangazi na wakati wa masika mara tatu. Amehimiza Kamati ya majosho kuwa waadilifu hasa katika matumizi ya fedha za uogeshaji. Mheshimiwa Theresia amesema kamati za majosho zisimamiwe na serikali ya kijiji kufungua account maalumu ya benki, waweka sahihi wawili watoke serikali ya kijiji na wawili kamati ya majosho. Mh. Theresia ameagiza kamati ya majosho kusoma taarifa za mapato na matumizi kwenye serikali ya kijiji. Fedha za majosho zitumike kuendeleza majosho na ratiba za uogeshaji zisiwe na upendeleo, ameelekeza watendaji kupanga utaratibu mzuri wa uogeshaji wa mifugo kwa vijiji visivyo na majosho. Mhe Theresia ameonya watu watakao hujumu miundo mbinu ya majosho hatua kali zitachukuliwa dhidi yao, ameelekeza kamati za vijiiji kusimamia ulinzi wa majosho.
Mheshimiwa Theresia amesema dawa za ruzuku zitakapoisha wafugaji waendelee kuchangia dawa. Amewaagiza maafisa mifugo pamoja kamati ya Majosho waandike taarifa za dawa wakati wa kubadilisha na taarifa ziende kwa mkurugenzi. Amewaonya wafugaji wanaokwepa kulipa mapato wakati wanapouza mifugo mnadani amesema Karatu itajengwa na wanakaratu wenyewe, ameomba Maafisa mifugo kutekeleza majukumu yao vizuri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa