Na Tegemeo Kastus
Vibanda mia mbili na thelathini na saba vilivyo katika eneo la soko kuu vitarudishwa Halmashauri ifikapo mwezi wa sita baada ya makubaliano ya mkataba kati ya Halmashauri na wananchi waliopangishwa vibanda hivyo kuisha.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya karatu ndg. Waziri Mourice wakati wa kikao cha baraza la bajeti ya mwaka ujao wa fedha. Amesema mikakati iliyojiwekea Halmashauri katika kukusanya mapato ni pamoja na kuweka kodi ya vibanda yenye uwiano sawa kwa vibanda vyote vinavyozunguka soko la Karatu. Kodi hiyo inatarajiwa kuanza kutozwa mwaka ujao wa fedha kadri itakavyoafikiwa kwenye kamati na baadae kupitishwa kwenye baraza. Amesema hali jinsi ilivyo; wafanyabiashara wenye vibanda 28 vya Mabucha wanalipa kodi tofauti na watu waliopanga katika vibanda 237 visivyo vya mabucha. Amesema mkataba walioufikia na Halmashauri wa kuendeleza vibanda 237vinavyozunguka soko ambao wanatozwa bei taafifu zaidi unaisha mwezi wa sita mwaka huu.
Amesema uwiano wa bei ya vibanda utaenda sawa hata kwa vibanda vipya vinavyoendelea kujengwa katika eneo la soko la Karatu. Amesema lengo ni kutoa uwiano sawa kwa wananchi wote wenye uhitaji wa kupangisha vibanda vya Halmashauri.
Ndg. Mouice amewapongeza madiwani kwa ushirikiano waliouonesha katika kupitisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha elfumbili na ishirini na moja, elfu mbili na ishirini na mbili. Amesema ni bajeti nzuri yenye vipaombele vienye kulenga kupeleka maendeleo kwa wananchi. Amesema watendaji wa Halmashauri wanawategemea waheshimiwa madiwani katika kuendesha shughuli za kila siku ndani na nje ya Halmashuri. Amesema jukumu kubwa la watendaji wa Halmashauri ni kuwashauri waheshimiwa madiwani.
Madiwani wakiwa katika kikao cha baraza cha kupitisha bajeti ya mwaka ujao wa fedha.
Naye Mh. Lolo Diwani wa Karatu ametoa ushauri vyumba 237 vya vibanda vya Halmashauri vinavyozunguka eneo la soko kodi yake iwe shilingi elfu hamsini kwa mwezi. Amesema lengo la kutoza kodi hiyo ni kusadia wananchi wanaofanya biashara katika vibanda hivyo. Amesema vibanda vya mabucha viendelee na kodi ya pango wanayolipa kwa sasa. Amesema lengo la kutoza kodi kwa kiwango hicho ni kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi.
Watendaji wakiwa katika kikao cha baraza ya kupitisha bajeti
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa