Mkuu wa wilaya ya Karatu, Mh. Abbas Kayanda amehitimisha mafunzo ya kumi ya jeshi la akiba katika kijiji cha Matala. Wanafunzi themanini na sita kati wanafunzi mia thelathini na sita ndio waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba kati yao wanawake ni wanne na wanaume ni sabini na saba.
Mh. Kayanda amewapongeza vijana kwa moyo wao wa uzalendo walioonesha katika kuitumikia nchi yao. Amesema katika kijiji cha Matala kumekuwa hakuna historia nzuri ya ulinzi na usalama hivyo mafunzo waliyopata vijana wa jeshi la akiba wayatumie vizuri katika kuimarisha ulinzi na usalama katika kijiji cha Matala. Serikali itatumia vijana hao waliomaliza mafunzo katika jeshi la akiba katika shughuli mbalimbali za kitaifa kama usimamizi wa mitihani na uchaguzi ili kupunguza gharama kubwa ta kuleta askari Mang’ola au Karatu kuja kufanya shughuli hizo.
Mh. Kayanda amewaasa vijana hao kutotumia vibaya mafunzo waliyoyapata na badala yake wazingatie misingi ya kiapo cha kwa kujikita katika kufanya kazi kwa kusimamia sheria bila kumuonea mtu au kufanya kazi kwa upendeleo. Akizungumzia kuhusu elimu Mh. Kayanda amesema shule zitafunguliwa mwezi wa kwanza tarehe kumi na moja amehimiza wazazi kuhakikisha watoto wote waliofaulu kwenda shule wanaenda shule na watoto wote waliofikia umri wa kuanza darasa la awali na darasa la kwanza wanakwenda shule. Ametoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha matala kuhakikisha mpaka tarehe kumi na nne mwezi wanafunzi wote wawe wameripoti shule kwa sababu serikali inatoa elimu bure hivyo mzazi hana kisingizio cha kutompeleka mtoto shule.
Akitoa taarifa yake kwa mgeni rasmi Mshauri wa Mgambo wilaya ya Karatu Kaptain Komba amesema mafunzo ya jeshi la akiba yamewasaidia vijana kupata elimu ya somo la uraia, mbinu mbalimbali za kivita, utimamu wa mwili elimu ya uhamiaji, elimu ya zimamoto. Amesema changamoto walizopata wakati wa kutekeleza mafunzo ya jeshi la akiba kwa vijana hao ni pamoja na wazee wa kimila kutowaruhusu vijana kushiriki mafunzo, utoro uliokithiri kwa wanafunzi wa mafunzo ya jeshi la akiba na matatizo ya kiafya.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa