Mpango mkakati wa kuboresha fursa za maeneo ya utalii ya ziwa Eyasi, na kuchangia maendeleo endelevu umewasilishwa katika Ukumbi wa Halmashauri. Mpango mkakati huo umesomwa ili kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa wataalamu wa Halmashauri na viongozi wa wilaya.
Mpango mkakati huo umeanzishwa kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Karatu unaendeshwa na UCRT na VSF ya Ubeligiji ili kuboresha usimamizi wa maeneo ya utalii kwa kufanya uchambuzi halisi kuangalia uwezo na udhaifu ili kupata mwelekeo wa kimkakati wa utalii kwa miaka mitano ijayo.
Mgeni rasmi katika uwasilishaji huo, Mhe. Theresia Mahongo amesema mpango wa utalii wa miaka mitano ni mzuri. Amesema mpango umegusa matatizo yote katika mpango mkakati wa kuboresha utalii wa Eyasi. Amesema ni vyema kuhamasisha watu juu ya mpango mkakati wa utalii ili tuweze kwenda wote kwa pamoja. Mhe. Theresia amesema tunapaswa tuwe na tafsiri nzuri ya uboreshaji utalii wa kitamaduni tunapowaeleza wananchi. Amesema ni vizuri viongozi tuwe na uelewa mmoja juu ya Mpango mkakati wa kuboresha utalii ili tuweze kujenga hoja za kuwafahamisha wananchi.
Naye Mbunge wa Karatu, Mhe. Willbroad Qambalo amesema sisi kama wadau, mpango mkakati huu si Msaafu wala Bibilia. Amesema tunaweza kujiwekea namna ya kufanya mapitio juu ya mpango mkakati huo kila mwaka kama kuna uhitaji wa kufanya marekebisho. Amesema baada ya kupitisha mpango mkakati huo sasa kwenye kuweka kanuni ndio kila mtu anayehusika na utalii wa utamaduni Tarafa ya Eyasi aje na hoja anahitaji kiasi gani kwenye tozo.
Mhe. Willbroad Qambalo wakati akichangia mjadala.
Mhe. Qambalo ameongeza kusema hali ikiendelea kama jinsi ilivyo sasa utalii wa kitamaduni utakufa Tarafa ya Eyasi. Amesema lazima tuende sawa, kuna kitongoji cha Murus kinapokea watalii sana na kuna kambi tatu za wahadzabe lakini hawajajumuishwa katika mpango huo. Kitongoji cha Murus hawapo Tarafa ya Eyasi lakini kina maeneo matatu mazuri yanayojihusisha vizuri na utalii wa kiutamaduni. Amesema mpango mzuri wa ardhi lazima utekelezwe, maeneo yale ya utalii yahifadhiwe ili wahadzabe wanaotegemea uwindaji waendelee na shughuli zao badala ya kusubiri utalii.
Katika uwasilishaji wa maoni, Mwenyekiti wa Halmahauri Mhe. Jublate Mnyenye amesema lazima tuweke utaratibu wa kupanda miti na kuacha shughuli za kuchoma mkaa na kukata miti hovyo. Amesema kwenye tozo, swala la kubadilisha fedha za kigeni, wenyeji watoe fedha za kitanzania na kwa wageni watumie malipo ya fedha za kigeni. Amesema waongoza utalii ukiwapa mwanya wa kutumia malipo ya fedha za kitanzania tutaweka mwanya kwa waongoza utalii kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni. Amesema upo umuhimu wa kuwashirikisha TATO katika mpango huu wa kuboresha utalii wa kitamaduni wilayani Karatu. Amesema Halmashauri ni msimamizi wa shughuli za utalii na shughuli za maendeleo, hatupaswi kuwatenga katika mpango mkakati.
Awali Ndugu Dismas Meitaya Program and Codinator UCRT -Ujamaa Community Resouce Team, wakati akiwasilisha amesema andiko lao limelenga kukuza utalii wa kitamduni unao adimika. Amesema mkakati umejikita katika Uhifadhi wa mazingira unaoboreshwa ustawi wa kiuchumi na na ubora wa maisha ya jamii.
Amesema wameangalia maadili ya tamaduni za kitalii na kuangalia vivutio vyote vya utalii Tarafa ya Eyasi, pamoja na pendekezo la malipo ya utalii. Amesema katika utafiti wa andiko wamebaini kumekuwa hakuna uhalisia katika uonyeshaji wa utamaduni. Amesema katika utafiti wameona kumekuwa na changamoto ya kukosa uwazi na uwajibikaji katika ukusanyaji wa mapato na kumekuwa na madhaifu ya miundo mbinu inayohusiana na shughuli za kitalii katika eneo la utamaduni wa kitalii. Amesema kumekuwa pia na tabia zisizo za kimaadili kwa waongoza utalii wa kijamii. Ndugu Dismass amesema rasimu mpango ikikubalika, utaandikwa vizuri ili uweze kusainiwa kama mpango makakati wa kuboresha utalii wa utamaduni Tarafa ya Eyasi.
Watendaji na Viongozi wakifuatilia uwasilishaji wa Mpango mkakati wa kuboresha utalii wa kitamaduni Tarafa ya EYasi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa