Waratibu wa afya waelekezwa kuandaa mpango kazi mzuri ambao utasaidia kuongeza idadi ya wananchi wanaojiunga mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboreshwa. Zoezi la kuratibu shughuli za uandikishaji lazima uhusishe viongozi wa siasa, viongozi wa dini na asasi za kiraia ili kujenga uelewa wapamoja kwa wananchi juu ya umuhimu wa kujiunga na bima ya afya ya jamii ulioboreshwa.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika kikao cha kamati ya afya ya msingi (DPHC) kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri. Mh. Kayanda amesema uandikishaji wa wananchi katika mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboreshwa bado uko chini, na uelewa wa watu juu umuhimu kujiunga na mfuko wa bima ya afya bado ni mdogo. Amesema wilaya ya Karatu ina kaya 45, 000 lakini kaya zilizojiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ni kaya 2600, amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anakuwa na uhakika wa matibabu. Mh. Kayanda amewapongeza wadau wa maendeleo shirika la food for his children kwa kusaidia kuandikisha katika mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboreshwa kaya 324 katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Mh. Kayanda akizungumza katika kikao cha kamati ya afya ya msingi
Mh. Kayanda amesema watu wanavyoozidi kujiunga na mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboreshwa unasaidia kujengea uwezo vituo vya afya katika kununua dawa. Ameongeza kusema ni vyema wataalamu wa afya wakainisha kwenye mbao za matangazo, aina za dawa zinazopatikana katika vituo vya afya ili kuondoa malalamiko juu ya ukosekanaji wa dawa katika vituo vya afya.
Mh. Kayanda ameelekeza wataalamu wa afya kufuata miongozo ya afya wakati dawa zinapoletwa kutoka bohari ya dawa (MSD) na kukabidhiwa kwenye vituo vya afya kwa kuhusisha kamati ya afya za vituo. Amesema wajumbe wa kamati hizo ndio wanasaidia kuelewesha wananchi juu hali ya upatikanaji wa dawa katika vituo vya afya. ameongeza kusema katika swala la utoaji wa dawa lazima taratibu za kujaza daftari la rejesta ya dawa ufuatwe, ili kuwezesha vituo vya kuwa na taarifa nzuri za matumizi ya dawa kwenye vituo lakini kusaidia kudhibiti vitendo vya upotevu wa dawa kwenye vituo.
Matukio katika picha wakati wa kikao
Akizungumzia kuhusu usafi wa mazingira ameelekeza watendaji kuja na mpango madhubuti wa kuhamasisha wananchi kujenga vyoo. Amesema ili kuongeza ufuatiliaji katika ujenzi wa vyoo bora ni lazima viongozi na watendaji wa ngazi zote kwenye maeneo yao ya utawala kuhusishwa vizuri katika kuweka msisitizo na kufanya ufuatiliaji.
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda amezungumzia juu ya usimamizi wa usafi katika mji wa Karatu ambao unafanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi. Ameelekeza juhudi zaidi zifanywe na wataalmu wa idara ya usafirishaji na mazingira ili kuweka mji wa Karatu katika hali ya usafi. Ameongeza kusema mji wa Karatu ni mji unaojihusiha na shughuli za utalii amesema lazima kuwe na mkakati maalumu wa kusimamia usafi na kuhakikisha mji unakaa katika hali ya usafi.
matukio katika picha wakati wa kikao cha kamati ya afya ya msingi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa