Wadau wa afya wilaya ya Karatu wanafanya mkutano wa siku mbili, kuanzia leo kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na sekta ya afya. Mkutano huo umefunguliwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Mhe. Theresia amewashukuru wadau wa afya BORESHA AFYA na wadau wengine kwa kujitoa kusaidia maswala ya afya. Amehimiza wadau wa afya kuendeleza mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU). Kwenye mapambano dhidi ya VVU tumejisahu ndio maana hatufanyi vizuri, amehimiza wadau wa afya kuendelea kupaza sauti ili kukabiliana na maambukizi vvu.
Mhe. Theresia amesema Karatu tunapata wageni wengi kutoka sehemu mbalimbali, ni vyema kuendelea kuwapa watu elimu juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi. Amesema shule ya sekondari ya Welwel ni shule ya kutwa na baada ya mida ya masomo wanafunzi wanarudi nyumbani. Zipo taarifa zinazoonyesha wanafunzi wa shule hiyo kujihusisha na tabia hatarishi. Amemuelekeza Mwenyekiti wa Halmashauri kuliangalia swala la shule ya sekondari welwel, tunawahitaji watoto hawa kwa ustawi wa taifa. Kuwapoteza watoto hawa ni hasara kwa taifa.
Mhe. Theresia amehimiza pia swala la elimu ya lishe, ameomba wadau wa afya kutoa elimu ya lishe mpaka shuleni. Kuna uelewa mdogo juu ya elimu lishe, tutoe elimu lishe kwa wakinama wanapoenda clinic ili wapate uelewa wa pamoja.
Mhe. Theresia amesema pia kuna uhitaji mkubwa wa elimu kwa wananchi juu ICHF iliyoboreshwa. Bima ni msaada mkubwa kwa wananchi, kwa sababu inawapa uhakika wa matibabu wananchi.
Awali katika taarifa yake Mganga Mkuu wa wilaya, Dkt Mustafa Waziri amesema wanachangamoto ya wakinamama kujifungulia nyumbani. Mwaka 2018 kama wilaya tulikuwa na kiwango cha 61 % ya kiwango cha wakinamama waliojifungulia katika vituo vya kutolea huduma na lengo la serikali ni kufikia 80%.
Dkt Mustafa amesema wanachangamoto pia katika swala la uzazi wa mpango, mwaka 2018 tulikuwa na kiwango cha 44 % na lengo la serikali ni kufikia 60%. Dkt.Mustafa amesema kuna kaya 45065 na kaya zilizojiunga mwaka 2018 ICHF iliyoboreshwa ni kaya 14255 ambayo ni sawa 31%. Changamoto kubwa ilikuwa ni kukosa vitendea kazi. Dkt Mustafa amesema mpaka sasa wamepokea simu 32 kwa vituo vyote 32 na watu watakohusika na undikishaji wameshateuliwa hivyo wanatarajia sasa kuongeza idadi ya watu watakao jiunga.
Dkt. Mustafa amesema upatikanaji wa dawa mwaka ( 2018 ) ulifikia 97.9 % , pia wameweza kukusanya damu salama chupa zaidi 1250. Amesema vituo vyote vya serikali na binafsi vinavyofanya operation vinatumia damu iliyokusanywa.
Wajumbe waliohudhuria kikao cha wadau wa afya.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha wadau wa afya.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa