Mafunzo ya uwezeshaji wa Tassaf yamefanyika wilayani Karatu, katika ukumbi wa ofisi ya Afisa tarafa wa tarafa ya Karatu. Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Maafisa waTassaf ngazi ya taifa yamejumuisha timu ya waelimishaji wa wilaya katika mafunzo hayo.
Kaimu mkurugenzi ndugu Godfrey Luguma amewashukuru wawezeshaji ngazi ya taifa wa Tassaf kwa kuleta elimu hiyo kwa vikundi vya uwekaji wa akiba na kuwekeza. Ndugu Luguma amesema elimu watakayopata walimu hao watakwenda kuelimisha vikundi katika ngazi ya vijiji. Amesema bila mafunzo madhubuti vikundi havitaweza kutimiza malengo ya kuazishwa kwake. Amewaomba waelimishaji wa Tassaf ngazi ya wilaya kuwa wasikivu na kuzingatia mafunzo hayo.
Ndugu Masejo Songo muwezeshaji kiongozi ngazi ya taifa amesema mafunzo haya yamelenga kuwawezesha walimu wa wilaya ili nao wapate kuwezesha kwenye vikundi ambavyo tayari vimeshajiunga na kuwekeza katika wilaya. Amesema hapo mwanzo vikundi vilikua vimeshapewa shajara kwa ajili ya kuweka akiba lakini wanavikundi hawakuwa na mafunzo ya undani ya namna ya kuwekeza na kuweka kumbukumbu. Ndugu Masejo amesema baada ya mafunzo hayo wawezeshaji wa wilaya watafanya mafunzo kwa vijiji vyote vya wilaya ya Karatu.
Waelimishwaji wakiwa wanafuatilia mafunzo kwa umakini.
Mwalimu kutoka wilayani Abdala Sichonge amesema awali walipokutana na vikundi walienda kuviunda tuu, lakini hawakuwa na elimu ya kuwapa wanavikundi ili waweze kujiendesha. Elimu waliyopata kutoka kwa wawezeshaji wa kitaifa, itafanya vikundi hivyo kuwa imara zaidi kwa sababu vikundi navyo vitapata elimu waliyopata kutoka kwa wawezeshaji wa kitaifa.
Mafunzo hayo pia yamewawezesha walimu ngazi ya wilaya kufahamu namna ya kutofautisha malengo ya muda mrefu na malengo ya muda mfupi. Lakini pia namna ya kupambanua na kuainisha malengo ya muda mfupi na malengo ya muda mrefu kwa wanavikundi. Mafunzo hayo yamewapa nafasi walimu wa ngazi ya wilaya kufahamu kanuni za uundaji wa vikundi pamoja na uelewa kwamba wananchi wanaingia kwenye vikundi vya uwekaji na uwezeshaji kwa hiari yao wenyewe.
Sheria za Vikundi vya uwekaji na uwezeshaji zinaundwa na wanakikundi wenyewe na kisha kupitiwa na Menyekiti na Mtendaji wa kijiji kabla ya kuwekwa sahihi. Maswala yote yanayohusu kikundi ya uwekaji na uwezeshaji yatajadiliwa kwenye kikundi husika na siyo nje ya kikundi. Fedha za kuanzisha vikundi vya kuweka na kuwekeza itatoka kenye vyanzo vya vikundi na hivyo, Tassaf itajihusisha na kutoa shajara. Lakini pia uongozi wa kikundi cha kuweka na kuwezesha utachaguliwa ka njia ya demokrasia.
Muwezeshaji akitoa maada kwa walimu wa vikundi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa