NA ALICE MAPUNDA
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Idd Kimanta, amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Ndugu Waziri Mourice, kuhakikisha ujenzi wa soko la Karatu unakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi huu wa tisa.
Ameyasema hayo alipokuwa akikagua ujenzi wa soko la Karatu linalotarajia kuchukua wafanyabiashara takribani 198. Mh. Kimanta amesema, soko hilo linatakiwa kuisha kabla msimu wa mvua haujaanza ili wafanyabiashara hao wapate mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao.
Soko hilo linauwezo wa kuchukua wafanyabiashara 202 na lenye hadhi nzuri ya kutoa nafasi ya kufanyia biashara kwa uhuru zaidi.
Mkuu wa Mkoa amekagua ujenzi wa soko hilo, ikiwa na moja ya shughuli anazozifanya katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Mh. Iddi Kimanta akikagua vizimba katika soko kuu Karatu,siku ya pili ya ziara yake wilayani Karatu
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa