Wafanyabishara wa wilaya ya Karatu, wamelalamika mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo juu ya ushrikishwaji duni wa kodi wanazotozwa katika maeneo yao ya biashara. Wamesema wao hawapingi kulipa kodi ila wanapaswa wajengewe ufahamu wa kulipa kodi hasa katika tozo na kodi mpya zinazoanzishwa.
Mhe. Theresia Mahongo alikuwa akipokea kero za wafanyabishara wa wilaya ya Karatu katika ukumbi wa Sumawe Complex Karatu. Kikao hicho kililenga kusikiliza na kutafutia ufumbuzi kero mbalimbali za wafanyabishara ili kutengeneza mazingira rafiki katika shughuli zao za kibiashara.
wafanyabiashara katika ukumbi wa Sumawe Complex wakifuatilia kwa makini mkutano
Mhe. Theresia amesema kikao cha mwisho walichokaa na wafanyabiashara ilikuwa mwezi wa tatu mwaka huu. Katika kikao hicho wafanyabishara walijadili kuhusu sekta ya kilimo juu ya gharama za uzalishaji kuwa kubwa kwa sababu ya kukosa elimu stahiki ya kilimo. Mhe. Theresia amesema katika kikao hicho walibaini matatizo ya kutofanya utafiti wa udongo ili kujua viwatilifu stahiki vya kutumia. Amesema haya yamesababishwa na wataalamu wa kilimo kutotimiza wajibu wao vyema katika kuwasaidia wananchi katika shughuli za kilimo.
Mhe. Theresia amesema katika kikao kilichopita kulikua na swala la elimu duni juu ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na vyakati ikiwa pamoja na mtaji. Gharama za pango umeme; gharama za maji, ushuru wa maeneo, ushuru wa mazao, gharama za utupaji taka, malipo kabla ya kuanza kufanya biashara, kuwa makubwa. Kikao hicho kilibaini pia wafanyabashara kukosa mkopo wenye riba nafuu. Katika sekta ya utalii kulikuwa na changamoto ya magari ya utalii kusimamishwa mara kwa mara na askari wa usalama wa barabarani.
Mhe Theresia amesema ili wafanyabiashara wafanye kazi vizuri lazima kuwe na mazingira ya amani. Amesema nchi isiyo na amani hakuna mazingira mazuri ya biashara, Mhe Theresia amesema katika hotel kubwa tayari ameshaelekeza wafanyabishara kufunga kamera za usalama. Mhe. Theresia amewatoa hofu wafanya biashara amesema nchi ina amani hivyo waendelee na biashara zao kama kawaida
Mhe.Theresia amewakumbusha wafanyabiashara umuhimu wa kulipa kodi. Amesema kunawatu hawalipi kodi jinsi invyopaswa, amesema hakuna taifa linalojengwa bila wananchi kulipa kodi. Amesema kuchelewa kulipa kodi kwa wakati, kunamsababisha mfanyabiashara kulipa kodi pamoja na adhabu ya kuchelewesha kulipa kodi kwa wakati (with interest). Amewaomba wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati amesema ana majina ya watu wasiolipa kodi inavyostahili. Mhe. Theresia amemuelekeza meneja wa TRA wa wilaya kutafuta mfumo rafiki wa kuwapa taarifa za kulipa kodi wafanyabiashara, amesema wanaweza kutumia ujumbe mfupi wa simu kwa wafanyabiashara ili waweze kukumbushwa pindi mda wa kulipa kodi unapofika Mhe. Theresia ameahidi pia kulipeleka swala la utitiri wa kodi ya misitu sehemu husika ili liweze kutatuliwa. swala hilo ni moja ya kero zilizoibuliwa na wafanyabiashara wa wilaya ya Karatu.
Awali katika kikao hicho mfanyabiashara Peter Masay amelalamikia juu ya utitiri wa kodi katika sekta ya misitu. Amesema katika biashara yake ya mbao anapata changamoto juu ya kodi nyingi wanazokabiliana nazo katika biashara ya mbao. Ndugu Peter amesema kuna kodi zaidi ya ishirini na moja katika idara ya misitu. Amesema kwenye eneo moja la biashara unalipa kodi, ulipe mashine ya kupasulia, ulipe kodi kwa ajili ya mbao, ulipe kodi ya mabanzi, bado kulipa kodi ya TRA, kuna kulipa kutokana na ulivyochukua mzigo lakini amesema kodi imekuwa haiangali mzunguko wa biashara.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa