Mafunzo ya kuwajengea uwezo wajasiriamali yamefunguliwa leo na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Mafunzo hayo ya siku moja yameendeshwa na kituo cha uwekezaji kanda ya kaskazini.
Mhe. Theresia amesema ipo nafasi ya uwekezaji wa kilimo, Karatu wananchi wanalima maua, mahindi, mbaazi vitunguu na matunda. Mhe. Amesema kuna fursa ya uwekezaaji wa kilimo cha mboga za majani, wawekezaji wa Hotel wananunua mboga za majani Arusha. Amesema amehamasisha kilimo cha alzeti wilayani Karatu, na kuna viwanda vidogo vidogo vya alzeti 12 lakini alzeti haitoshi. Viwanda huwa vinafungwa ikifika mwezi wa tisa kwa sababu ya kukosa malighafi, alizeti nyingi inanunuliwa kutoka singida.
Mhe Theresia amesema kuna zao la vitunguu Mang’ola, tumewekeza kwenye ghala ili vitunguu viongeze thamani kwa mkulima. Ghala limejegwa na serikali kwa gharama ya billion 1.5, lakini wanaoweka vitunguu ni watu kutoka Kenya. Soko la vitunguu Mang’ola limewekwa ili kusaidia wakulima wanufaike na bei ya zao la vitungu, ni vyema wananchi walitumie Ghala hilo. Vitunguu viuzwe kwenye ujazo unaotakiwa, amesema tabia ya kujaza rumbesa imerejea tena wafanyabiashara wanaofanya hivyo waache mara moja. Kufanya hivyo ni kuwanyonya wakulima, Mhe. Theresia amewaelekeza watu wa vipimo soko la Ngarenaro katika kikao cha ushauri wa mkoa juu ya adha hiyo. Amesema vitungu vinaweza kuongezwa thamani zaidi kwa kuweka grade na kuvifanyia sorting. Mhe. Theresia ameomba watu kuwekeza kwenye kilimo cha vitungu. Tarafa ya eyasi kuna fursa ya kilimo cha umwagiliaji na serikali imeweka mpango wa kujenga visima ili kuendeleza kilimo cha umwagiliaji.
Mhe. Theresia amesema kuna fursa nzuri ya kuwekeza kwenye mbaazi, tulime mbaazi na tuanzishe viwanda vya mbaazi. Mbaazi hutumika kutengeneza biskuti, mbaazi inaweza kuongeza thamani kwa kutengeneza vitu vingine vinavyotegemea mbaazi. Hasa wakati huu ambao soko la mbaazi nchini India halipo.
Mhe. Theresia amesema kuna samaki kutoka ziwa Eyasi wanapatikana samaki watamu sanaa. Kuna wakati ziwa linapungua wanabaki samaki wadogo na magadi samaki hao ni rahisi kuwapata pia ni wazuri sana, ni fursa kwa muwekezaji kuwekeza kwenye chakula cha mifugo.
Mhe. Theresia amesema kuna kahawa iliyo bora first class inayopatikana Karatu, wananchi wa Burger wamehamasika kuanza kulima kilimo cha kahawa. Amesema wakulima wakubwa wanatoa mbegu za kahawa bure kwa wakulima wadogo. Amesema kahawa yetu inalimwa katika nyanda za juu, ndio maana inakuwa ina ladha nzuri. kahawa siyo tu kwa ajili ya kuuza nje inaweza ikatumiwa kwa matumizi yetu nyumbani. Mhe Theresia amesema ni vyema wakulima wakubwa wakawekeza kwenye viwanda vikubwa vya kahawa.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa