Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi yamefanyika kwa maandamano ya amani na kupokelewa na Mhe. Theresia Mahongo Mkuu wa wilaya ya Karatu katika uwanja wa mazingira bora. Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wafanyakazi ni “ Tanzania ya uchumi wa kati inawezekana, wakati wa mishahara bora kwa wafanyakazi ni sasa.
Mhe. Theresia amewapa zawadi watumishi waliofanya kazi vizuri katika maeneo yao ya kazi, na amewapongeza waajiri kwa kutoa motisha kwa wafanyakazi. Mhe Theresia amewaelekeza waajiri kulipa kwa wakati mifuko ya hifadhi ya jamii kwa watumishi. Amewataka waajiri kulipa madeni ya watumishi, amesema malalamiko ya watumishi kutolipiwa na wajiri wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii yanaongezeka. Mhe Theresia ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi mtendaji wa wilaya kutoa barua za miongozo ya kazi (job description) kwa watumishi wote ili watu wajue wajibu wao katika maeneo yao ya kazi.
Mhe. Theresia amesema serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwenye maeneo ya kazi kwa kuhakikisha mishara ya wafanyakazi inalipwa mapema, amesema kwa mkoa wa Arusha serikali inalipa billion 179 mshahara wa wafanyakazi. Serikali imeajiri watumishi na Karatu imepata walimu wapya 27 na madaktari 32 kwa mwaka huu wa fedha. Serikali kwa mwaka wa fedha 2017-2018 imepandisha madaraja watumishi 1017 kati yao walimu ni 750. Mwaka wa fedha 2018-2019 serikali itapandisha madaraja watumishi 2132 kati yao walimu ni 1542. Serikali imelipa madeni ya walimu mwezi February na March mwaka huu shilingi million 52 posho za uhamisho pamoja na likizo.
Mhe. Theresia amewataka watumishi kutoa huduma bora kwa wananchi, kwa taarifa zinazotolewa na Takukuru bado Halmashauri, Mahakama zinaongoza kwa rushwa. Amewataka wafanyakazi kupambana ili kutoa haki kwa wale wanaowahudumia, hakuna haki bila wajibu. Mhe. Theresia amesema mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa serikali za mitaa, amewataka watumishi kusimamia zoezi hilo vyema kwa kuwapa wananchi elimu juu ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Amewashukuru watumishi kwa kuendelea kulinda amani ameomba watumishi kuendelea kuwa na subira, juu ya ongezeko la kima cha mishahara amesema subira yavuta kheri.
Katika risala ya wafanyakazi iliyosomwa na ndugu Florence Mollel, wameomba serikali, kupunguza utofauti mkubwa wa maslahi kati ya mtumishi wa ngazi ya chini na mtumishi wa ngazi ya juu. Amesema maslahi ya kazi za kisiasa yamekuwa mazuri zaidi ya watendaji wa kawaida wa serikali. Hii imefanya wataalamu wengi kufikiria kwenda kwenye shughuli za kisiasa na hivyo kuathiri shughuli za kitaalamu.
Ndugu Florence amesema uingiliano wa siasa kwenye utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo ambao unakwamisha sera za serikali, dira maendeleo 2020-2025, Maendeleo endelevu ya 2030 na Mipango ya mandeleo ya miaka 5 na ilani ya chama cha mapinduzi ya 2015-2020 kuathiriwa wakati wa utendaji.
wafanyakazi wakifuatilia kwa makini maadhimisho ya may mosi Uwanja wa Mazingira Bora.
Mmoja wa wafanyakazi aliyepewa zawadi ya may mosi Uwanja wa mazingira Bora.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa