NA TEGEMEO KASTUS
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda ameridhishwa na ujenzi wa nyumba ya mganga na Muuguzi iliyojengwa katika zahanati ya Ngaibara. Kabla ya ujenzi wa nyumba hiyo two in one wauguzi na daktari walikuwa wanaishi nje eneo ilipojengwa zahanati.
Hayo yamesemwa Mh. Kayanda alipokuwa akielekeza juu ya uboreshaji wa huduma za afya katika zahanati hiyo. Amesema Mganga pamoja na wauguzi wanapaswa kuanza kutumia nyumba hiyo ili waweze kuhudumia wagonjwa pindi inapotokea dharura nje ya wakati wa kazi. Wakati huo huo Mh.Kayanda ameelekeza uwekaji wa Marumaru umalizike haraka ili huduma za afya ziendelee kama kawaida katika zahanati ya Ngaibara.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika eneo la ujenzi wa maabara kituo cha afya Endabash
Mh. Kayanda ametembelea kituo cha afya Endabash na kujionea uwekaji wa jamvi unaoendelea kwa siku ya pili katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi unaolenga kuimarisha miundo mbinu katika sekta ya afya. Ujenzi wa jengo la maabara ukikamilika utasaidia kuimarisha huduma za utoaji wa afya katika kituo cha afya Endabash.
Mh. Kayanda ametembelea mradi wa ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Qaru ambayo yapo katika hatua za uchimbaji wa msingi. Fedha za ujenzi wa madarasa hayo zimetolewa na EP4R, na Mpaka sasa ukusanyaji wa mawe na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa msingi umefanyika. Ujenzi wa madarasa hayo unatarajiwa kufanyika ndani ya kipindi kisichozidi siku tisini( miezi mitatu)
Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda katika eneo la ujenzi wa madarasa mawili shule ya sekondari Qaru.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa