Na Tegemeo Kastus
Mkataba` wa wakulima wa ngano na wakala wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kanda ya kaskazini uandikwe kwa Kiswahili ili kila mtu asome na kuuelewa. Kabla ya kusainiwa kwa mkataba ni lazima upitiwe na mwanasheria wa Halmashauri akiwa na wajumbe wa pande zote mbili wa chama cha ushirika na bodi ili kujiridhisha kama mkataba unatija kwa pande zote.
Mh. Abbas Kayanda amesema hayo wakati alipofanya mkutano na wakulima wa ngano wilayani Karatu katika Ukumbi wa Halmashauri. Amesema maafisa ugani lazima watoke ofisini na wagawane maeneo ya kwenda kusaidia wakulima namna bora ya kufanya kilimo cha kisasa, ikiwa ni pamoja kuanzisha mashamba darasa ya ngano na kufanya ufuatiliaji kwa wakulima mara kwa mara.
Mh. Kayanda ameelekeza Maafisa ushirika kufufua vyama vya ushirika kwenye maeneo ambayo vyama vya ushirika vimekufa. Amesema lazima vyama vya ushirika vianzishwe na viweze kuimarishwa ili wakulima waweze kunufaika kwa kupata mkopo. Ameomba wakulima kuzingatia maelekezo waliyopewa na wataalamu ili waweze kujikita katika uzalishaji wa kilimo cha ngano chenye tija na kuepukana na ubadhilifu. Amesema wakulima watakofanya udanganyifu hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa sababu watakuwa wanaharibu sifa nzuri tulionayo wakulima wa Karatu kwenye kilimo cha ngano.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda ( wa kwanza kushoto) akizungumza na wakulima wa ngano
Mh. Kayanda ameomba wananchi kuacha kuchakachua mbegu za ngano jambo ambalo linasababisha kushindwa kupata ngano inayokubalika na wenye makampuni. Amesema hii ni fursa kwa wakulima kuongeza kiasi cha ngano ianayozalishwa nchini kwasababu soko la uhakika limepatikana. Amesema serikali kupitia wizara ya kilimo imedhamiria kufufua kilimo cha ngano, sasa bei ya kilo moja ya ngano itanunuliwa kwa Tsh. 800 kutoka Tsh 650.
Meneja wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kanda ya kaskazini ndg. Hiza Kiluwasha amesema lazima wakulima kufanya kilimo chenye tija na kwa kupanda mbegu bora na kufuta maelezo ya maafisa ugani. Amesema mkulima akipanda mbegu bora za ngano na mkulima kwa kufuata maelekezo ya wataalamu, ya kuandaa shamba, kutumia mbolea sahihi, na dawa sahihi kwa wakati muafaka mkulima anauwezo wa kupata gunia 12 kwa hekari na kuendelea. Hivyo wakulima wadogo na wakulima wakubwa ni vyema kujiunga na vyama vya ushirika. Vyama vya ushirika vilivyo hakikiwa na mrajisi ndivyo vitakavyoingia mkataba na bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kwa ajili ya kusambaziwa mbegu.
Ndg. Kiluwasha amesema utaratibu utakaotumika sasa mbegu za ngano zitasambazwa kupitia vyama vya ushirika kwa wakulima wadogo isipokuwa kwa wakulima wakubwa kuanzia hekari 50 ambao watachukuliwa mmoja mmoja. Mkataba ambao chama cha ushirika itakaoingia na wakala wa bodi ya nafaka ndio utasaidia vyama vya ushirika kununua ngano. Amesema vyama vya ushirika ndivyo vitakavyolipwa na kuja kulipa wakulima.
picha za matukio tofauti wakati wa kikao cha wakulima wa ngano na Mh. Abbas Kayanda
Meneja wa shirika la bima ya taifa mazao Mkoa wa Arusha ndg. John Mdenye amesema kuna bima ya mkopo atakaopata mkulima. Amesema huwa bima hiyo inasaidia kumlipa mkulima mkopaji pindi anapopata tatizo litakalomfanya asiweze kulipa mkopo. Amesema wameweka bima hyo kwa sababu kuna sababu mbalimbali kama kuugua kifo zinazomfanya mkulima aliyekata bima ya mkopo kushindwa kulipa.
Amesema kuna bima ya mazao kwa mkulima kwa mambo ambayo yapo nje ya uwezo wa mkulima, amesema bima hii inamasaidia kwenye changamoto ya ukame mabadiliko ya hali ya hewa yanayosababisha mafuriko, upepo unaoharibu mazao, magonjwa ya mazao au wadudu ambao hawana dawa. Mkulima anapaswa kuleta mapatao yanayopatikana kutokana mauzo ya mazao kwenye shamba lake lakini pia gharama za uazalishaji.
Mkulima wa ngano ndg. John Tippe ameshukuru serikali kwa mapango wa kuboresha kilimo cha ngano. Amesema serikali itengeneze mbegu za kutosha za ngano ili kupunguza gharama za kuchukua mbegu kutoka nje ya nchi. Amesema kuchukua mbegu nje ya nchi ni kunufaisha nchi nyingine, amesema sasa serikali ifikirie namna ya kuwapa mikopo wakulima wadogo wadogo ili waweze kuwa na zana za kisasa za kilimo.
Matukio tofauti tofauti katika picha wakati wa kikao
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa