Wafanyabiashara wamemueleza Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe Theresia Mahongo kwamba soko la mazao ya kilimo limedorora. Kero hizo zimetolewa na wafanyabiashara wa wilaya ya Karatu katika kikao cha wafanyabiashara kilichowahusisha watendaji mbalimbali wa Halmashauri. kikao kililenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku ili kuwajengea mazingira rafiki ya kufanya biashara.
Mhe. Thresia Mahongo amesema kuna haja ya kufanya utafiti tena Mang’ola juu ya kupungua uzalishaji wa vitunguu. Mhe. Theresia amesema upo umuhimu wa wakulima pia kufuata maelezo kitaalamu katika kujihusisha na kilimo cha kisasa. Kupuuzia maelelekezo ya kitaalamu katika kufanya shughuli za kilimo kunasababisha uzalishaji wa nafaka kupungua. Mhe. Theresia Mahongo amesema swala hilo bado linafanyiwa kazi, ili liweze kupatiwa ufumbuzi wa kina juu ya kupungua uzalishaji wa vitunguu Mang'ola. Mhe. Theresia amesema amelichukua swala la viwanda vya ndani kukwepa kununua ngano inayolimwa na wakulima wa ndani jambo linalofanya wakulima wa ngano kukosa soko la uhakika la zao la ngano. Ngano hutumika kutengeneza mikate lakini pia sankisti lakini baadhi ya vinywaji, makapuni ya ndani yamekuwa yakinunua zao hilo kutoka nje ya nchi.
wafanyabiashara wakifuatailia ajenda za kikao kwa makini katika ukumbi wa Sumawe complex Karatu.
Ndugu Paulo Jackobo Afisa bishara wa wilaya amesema kuna udalali mkubwa unaofanywa kwa wakulima wa vitungu Mang’ola wakati wa ununuzi wa vitunguu. hali inayosababisha wakulima kukosa bei nzuri ya vitungu pindi wanapouza. Ndugu Jackobo amesema ujazo sahihi wa gunia ni kilo 100 na siyo zaidi ya hapo lakini wakati wa ununuzi wafanyabishara wanakuja na vifungashio vienye ujazo mkubwa zaidi ya kipimo elekezi. Licha ya elimu kutolewa kwa wakulima juu ya kuepuka kufunga rumbesa ili wasinyonywe na wachuuzi wakulima wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wakati wa uzaji wa vitunguu. Ndugu Jackobo Amesema Halmashauri imejipanga kutuma wataalamu Nairobi Kenya na Uganda ili kukutana na wanunuzi wakubwa wa vitunguu na wawaunganishe moja kwa moja na wakulima wa vitunguu. Lengo likiwa ni kuondoa udalali unaofanywa kwa wakulima wa vitunguu Mang’ola ili waweze kunufaika na kilimo.
Awali ndugu Zakaria Qamara amemueleza mkuu wa wilaya kwamba kikundi cha kulima ngano na shairi wanamalengo ya kujenga kiwanda cha ngano na shairi. Lakini kutokana na hali ya hewa kubadilika imefanya mazingira ya uendelezaji wa kilimo kutokuwa rafiki.Amesema watu wameacha kulima ngano kwa sababu hakuna soko zuri linalowanufaisha wakulima. Ngano inatumika kutengenezea sankisti na mikate.
Ndugu Qamara amesema kuna tatizo la makampuni makubwa kununua ngano kutoka nje ya nchi na kuacha ngano inayolimwa ndani. Wamesema wao kilimo ndio uti wa mgongo, wameomba kupewa elimu nzuri ya kilimo ili waweze kuzalisha ngano yenye ubora. Lakini pia wameomba kuzuia makapuni makubwa kununua ngano kutoka nje na kuiacha ngano inayolimwa Tanzania. Lakini pia amezungumzia swala la Mang’ola namna uzalishaji wa vitunguu ulivyopungua; ndugu Qamara amezungumzia pia soko la Mang’ola la vitunguu ambalo nalo limekosa ufanisi, katika kusaidia wakulima kupata bei nzuri ya zao la vitunguu . Amewaomba wataalamu wa kilimo waweze kusaidia kuboresha uzalishaji kama awali na kupata soko la uhakika la mazao yao. .
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa