Afisa elimu sekondari Bi, Kalista Maina ameendelea na ziara yake ya kutembelea shule za sekondari wilayani karatu. Ziara yake imelenga kujionea utendaji kazi wa walimu pamoja na kutambua kero za kitaaluma katika maeneo yao ya utendaji kazi.
katika ziara yake shule ya sekondari Florian amesema shule hiyo imezidi kushuka kitaaluma ukilinganisha na matokeo ya awali ya mtihani wa moko waliofanya. Shule hiyo ni shule ya 27 kati ya shule 32 za wilaya. Shule ya sekondari Florian haina ufaulu wa daraja la kwanza wala daraja la pili, ufaulu umeanza daraja la tatu. Matokeo haya kuanzia shule ya sekondari ya Welwel ambayo imekuwa ya 20 mpaka shule ya 32, waalimu wanaofundisha kidato cha nne katika shule hizo waandike barua kwa mwajiri kujieleza wamejipanga kwa namna gani kuinua ufaulu. Walimu 3 waliopata daraja âFâ ambao ni mwalimu wa bailojia, fizikia, na hesabu wataitwa kujieleza kwa muajiri, knamna watakavyo ondoa "F" na kuongeza ufaulu matokeo ya kidato cha nne.
Bi, Maina amesema shule ya sekondari Florian ni shule kubwa, haiendani na hadhi ya ufaulu duni uliojitokeza kwa mtihani wa moko kidato cha nne. Ametoa maagizo kwa walimu wa shule hiyo kujipanga kwa kipindi cha miezi mitatu ili kupata matokeo mazuri kwenye mtihani wa taifa. Amewakumbusha muundo wa mtihani wa taifa ulivyobadilika na ametoa maelekezo kwa walimu kuwapa wanafunzi mazoezi ya mitihani kulingana na muundo huo wa mtihani.
Bi, Maina amesema kuwapa wanafunzi mazoezi ya maswali kunamsaidia mwalimu hata namna ya kufundisha kwa sababu kuna wakati mitaala yetu ilibadilishwa na kuletwa nyingine. Bado kuna mambo ambayo hayapo kwenye mitaala mpya ila yanatoka kwenye mtihani kwa mfumo wa mitaala ya zamani. Bi, Maina amesema mazoezi mengi maswali yanasaidia mwalimu kuandaa vyema andalio la somo kulingana na mahitaji. Ameongeza kusema maneno mahususi yanayotumika kwenye mtihani yanamsaidia mwalimu kuandaa maudhui yanayoendana na somo husika.
Afisa elimu taaluma ndugu Robert Sijaona amesema kwa ukaguzi walioufanya wameona kuna ukwepaji wa kufundisha masomo kwa kiasi kikubwa sana. Amesema kwa kidato cha kwanza mkondo âAâ pekee kuna vipindi 159 vya masomo tofauti tofauti ambavyo havijafundishwa. Sasa ni wakati wa kubadilika kiutendaji, walimu hatuzingatii misingi ya taaluma yetu. Kuna ujazaji shajara ambao haufuati utaratibu, amesema shajara zilizojazawa nyingi hazijawekwa saini na mkuu wa shuke wala mwalimu wa taaluma. Amesema hii inaonesha wadhibiti ubora wa ndani ya shule hawatekelezi majukumu yao vizuri jambo linalodumaza maendeleo ya taaluma. Shule imeanguka kwa nafasi 50 kwenda chini, mwaka jana ilishika nafasi ya 155 katika matokeo ya moko na mwaka huu imeshika nafasi ya 206 kati ya shule 226. Tufanye kazi zetu vizuri na tuzingatie taratibu, vitu vilivyowekwa ni msingi wa ufundishaji ambao unaleta matokeo chanya kwa wanafunzi. Amesema shule kongwe yenye kidato cha tano na sita haipaswi kuwa na ufaulu duni kiasi hicho.
Ndugu Robert Sijaona amesema lazima walimu tufundishe kwa malengo na hatuwezi kufundisha kwa malengo bila kufuata utaratibu. amesema kwenye kuandaa andalio la somo kuna vitu vinabadilika kila siku, lazima sasa walimu waliopata semina Karatu sekondari juu ya namna ya kuandaa andalio watoe elimu hiyo kwa wenzao. Ametoa maalekezo kwa walimu waliopata semina kuaanda andalio la kazi, kutenga siku kwa ajili ya kuelekeza walimu wenzao.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa