Afisa mwandikishaji wa ngazi ya jimbo ndugu Waziri Mourice amewashukuru wafanyakazi walioendesha zoezi la uandikishaji wa maboresho ya daftari la wapiga kura. Wafanyakazi hao wa muda wamekusanyika Halmashauri kukabidhi vifaa vya BVR, takwimu za uandikishaji kwa maafisa wa tume, pamoja na kupewa stahiki zao.
Ndugu waziri mourice amesema amezunguka vituo 186 kati ya vituo 222 vilivyowekwa kwa ajili ya kujiandikisha, ametembelea Tarafa ya Mbulumbulu, Tarafa ya Eyasi, Tarafa ya Endabash na Tarafa ya Karatu. Amejionea kazi jinsi ilivyofanyika kwa umakini na juhudi kubwa na amejionea na kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji.
Ndugu Waziri amesema kuna maeneo mengine yalikuwa na hali ngumu kiutendaji hakuna chakula, barabara ni mbovu lakini bado kazi imefanyika. Amesema kuna maeneno hata ukiwa na fedha huwezi kununua chakula, na maeneo mengine hata kufanya mawasiliano ya simu haiwezekani. Amewashukuru sana kwa utendaji kazi wao kwa sababu wangeweza kukataa kufanya kazi na kukwamisha zoezi la uandikishaji. Amepongeza watumishi hao pia kwa kuhifadhi vifaa vya BVR KIT kwa usalama mkubwa. Hakuna kifaa kilichoharibika wakati wa zoezi hilo wala kuibiwa jambo ambalo linatoa taswira na sifa nzuri kwa Halmashauri.
BVRT OPERATORS wakikaguliwa vifaa vyao kabla ya kuvikabidhi kwa maafisa wa tume.
Ndugu waziri Mourice amesema ameandika mawasiliano ya watendaji kazi wote ili zoezi jingine likijitokeza wapewe nafasi. Ameshukuru waandikishaji kwa kumpa sifa kubwa kwa kazi nzuri waliyofanya kwenye zoezi la maboresho la wapiga kura. Amesema kwa uungwana waliofanya wamemvisha nguo na kupokea sifa ambazo wao walistahili kuzipata. Amesema moyo walioonesha katika kazi hiyo ndio uliofanya zoezi kwenda vizuri. Ameongeza kusema kama mwandikishaji au BVR OPERATOR angeaamua kuacha kazi tayari zoezi lingeingia dosari. Amewaomba wafanyakazi hao wa muda kuomba nafasi za kazi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka unaokuja. Amewaambia ameshaweka kazi data (data base) ya watu wote waliofanyakazi katika zoezi hilo ili wawape kipaombele.
Ndugu Waziri Mourice amewapa siku moja ya mapumziko walimu wote walioshiriki katika uandikishaji wa zoezi hilo kwa kazi ngumu waliokuwa wakiifanya.Amefanya hivyo kuthamini mchango wao wa kazi katika zoezi hilo. Amewaahidi wafanyakazi wengine ambao si watumishi wa serikali kuwaandikia barua ya udhamini pindi watakapopata ajira sehemu yeyote na wakahitaji mdhamini. Amewaasa kutokata tama katika majukumu yao ya kila siku, amesema kila kitu kinawezekana pindi unapojituma na kuweka nia.
Maafisa waandikishaji wakikabidhi nyaraka mbalimbali Halmashauri baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa