Afisa elimu sekondari Karatu ameendelea na ziara yake ya kukagua mikakati yake ishirini na tano aliyotoa maelekezo kwa walimu. katika ziara yake shule ya sekondari Ganako amefuatilia maendeleo ya kitaalmu ya wanafunzi pamoja na hali ya ufaulu wa matokeo ya moko kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
Afisa elimu Bi, Kalista Maina amesikitishwa na kitendo cha walimu kutojaza maandalio ya masomo pamoja na udhaifu wa kuwapa watoto mazoezi pindi wanapomaliza mada za masomo. Ametoa muda wa mwezi mmoja kwa walimu ambao hawajajaza maandalio ya somo kuhakikisha mpaka inapofika mwezi wa nane tarehe thelathini wawe wameshajaza na kuleta maaandalio hayo ya somo ofisini kwa afisa elimu. Maagizo hayo yamekuja baada ya kutembelea shule hiyo na kukuta walimu wamejaza maandalio ya somo nusu nusu na kwa kuruka na baadhi yao kutokuwa nayo kabisa.
Bi. Maina amesema kwa walimu wanaofundisha darasa moja lenye mikondo mingi, wanaweza kutumia andalio moja la somo kwa maana ya maudhui “concept” kufundisha mikondo yote. Ametoa maelekezo katika ujazaji wa andalio la somo ambao kuna mabadiliko kidogo katika kujaza kipengele cha kujaza tathimini “assessment” ametoa wito kwa walimu kufuatilia ili kufahamu mabadiliko hayo.
Afisa elimu sekondari akiwa na watendaji wenzake wa idara ya elimu katika zoezi la ukaguzi '
Bi, Kalista amesema shule hiyo imeanguka kwa nafasi sitini mtihani wa moko kimkoa ukilinganisha na ufaulu wa mtihani huo mwaka uliopita. Shule imekuwa ya ishirini na nne kati ya shule thelathini na mbili za wilaya ya Karatu. Amesema ufaulu wa shule zote zilizopo katikati ya mji ni duni ukilinganisha na shule zilizo pembezoni. Ametoa maelekezo walimu kujituma na kubadili matokeo hayo, amesema imezoeleka shule za sekondari za mjini ndizo zinazoongoza kwa kufaulisha wanafunzi vizuri. Karatu hali imebadilika walimu walio pembezoni mwa wilaya ndio wanaofundisha na kufaulisha vizuri kuliko walimu wa mjini. Bi, Kalista amesema shule ya Baray imefanya vizuri na ndio shule inayoongoza kwa shule za serikali kwa kuwa na matokeo mazuri ya mtihani wa moko. Bi, Kalista amesema kuna walimu wanaofanya vizuri ambao ninaona jitihada zao katika ufundishaji akitoa mfano mwalimu wa somo la kemia shule ya sekondari Mang’ola mwenye ufaulu wa alama A tano na F mbili ambazo nazo ameahidi kuzitoa katika matokeo ya mwisho wa mtihani wa kidato cha nne.
Bi kalista amesema ikifika mwezi wa kwanza kama matokeo hayatabadilika atabadlisha walimu wote wa shule zilizofanya vibaya mjini. Amesema haiwezekani mwalimu ukae mjini upate nyenzo zote na bado ufaulu uwe duni, wakati walimu wenye taaluma hiyo hiyo waliopo pembezoni wanafaulisha vizuri wanafunzi. Bi, Maina amesema Ganako inaufulu mzuri wa wanafunzi wanaosoma kidato cha tano na sita na ndio shule inayoongoza kwa ufaulu mzuri kwa kidato cha sita. Amehoji kwanini walimu wanaofundisha kidato cha kwanza mpaka cha nne wasipate matokeo mazuri kama wanayopata walimu wa kidato cha tano na sita. Amesema udhaifu wa kutofutilia taratibu za kujaza maandalio ya masomo shajara kukosa kufidia vipindi ambavyo havijafundishwa na, kutotoa mazoezi, kuangalia notisi za wanafunzi na kusahihisha ndio kunaleta matokeo hayo mabaya.
Naye Afisa Elimu Taaluma Ndugu Robert Sijaona amesema tatizo la walimu kutokagua notsi za wanafunzi limekuwa kubwa. Kuna makosa watoto wanafanya wakati wa kunakili, ni jukumu la mwalimu kukagua na kuondoa dosari zinazojitokeza kwenye notsi. Amesema katika ukaguzi waliofanya kuna madaftari wanafunzi wamechora michoro kwa makosa. Amesema makosa hayo ndio mtoto anayo nukuu na kujibia mitihani.
afisa elimu skondari na watendaji wa idara wakikagua madaftari ya mzoezi, na faili la akiba ya maswali
Ndugu Sijaona amesema kuna tatizo pia la walimu kuchelewa kuingia darasani wakati wa vipindi au kuwahi kutoka kabla ya muda wa kipindi kuisha. Ndugu Sijaona amesema utendaji wa kazi kwa baadhi ya walimu sio mzuri, walimu wameshindwa kuonesha tija ya kazi. Amesema tabia zinazo zoretesha taaluma, jamii inaziona na jamii inazilalamikia. Amewaasa walimu kutambua majukumu yao waliyoyapewa ya kufundisha, amesema kuna watu wanaomba ruhusa nyingi ambazo zinaleta mashaka. Amesema lazima turudishe heshima ya kufaulisha wanafunzi vizuri shule ya Ganako.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa