NA TEGEMEO KASTUS
Proper preparation prevents poor performance hiyo ndiyo fomula ambayo wanafunzi wameusiwa kutumia ili kuepuka kupata matokeo ambayo hayaridhishi katika mtihani wa kitaifa wa kumaliza kidato cha sita mwaka huu.
Afisa elimu sekondari Bi, Kalista maina amesema hayo wakati wa akiwakabidhi wanafunzi, vyeti vya kuhitimu elimu ya sekondari kidato cha sita. Amesema anaimani kabisa wanafunzi wa Karatu sekondari wamejiandaa vizuri. Mtihani ni vita kati ya Muandaaji na anayeenda kufanya mtihani, lazima mwanafunzi ujiamini katika pambano kwamba unaenda kushinda, amehimiza wanafunzi kusoma swali na kulielewa linahitaji nini kabla ya kuanza kujibu.
Amehimiza wanafunzi kuzingatia muda wa kujibu maswali na kumaliza kwa wakati, lakini kuangalia maswali mepesi na mswali yenye alama nyingi. Amesema mathalani unajibu swali la essay fuata utaratibu wa kujibu swali la essay kulingana na matwakwa ya swali.
Bi. Maina amewapongeza walimu wa sekondari ya Karatu amesema ni walimu wa pekee sana na wamejitoa mpaka hatua ya wanafunzi kumaliza kidato cha sita. Wamemaliza mada za darasani na wanafunzi wamepata muda wa kurudia vizuri tayari kwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha sita.
Amesema anaimani kubwa na shule ya sekondari Karatu wanafunzi wengi wataenda vyuo vikuu. Amesema kumekuwa na usumbufu mkubwa wa wazazi wanaotaka kuhamashia watoto shule ya sekondari Karatu. Karatu sekondari imetokea kupendwa sana kipindi cha hivi karibuni kutokana na kuwa na walimu mabingwa wa kufundisha, wanaojikita katika ujuzi walionao vizuri katika kuandaa wanafunzi.
Bi, Maina amesema anao wakuu wa shule 35 lakini mkuu wa shule ya sekondari Karatu ameng’ara sana katika uongozi wake. Amesema mkuu wa shule anakarama ya uongozi ameongeza kusema ni mwalimu anayemtanguliza Mungu katika utendaji wake wa kazi. Amesema muda si mrefu atahitaji walimu watano kuwa wakuu wa shule ili wamsaidie katika kujenga uwezo wa kitaaluma shule nyingine za sekondari katika wilaya ya Karatu.
Amesema shule ya sekondari Karatu nidhamu ipo juu sana, kuanzia Mkuu wa shule mpaka kwa walimu. Lakini ukitizama hata namna wanafunzi walivyo vyaa unagundua wamejengwa katika misingi ya kinidhamu hakuna wanafunzi waliovaa suruali zilizobana au kunyoa mitindo ya ajabu. Amesema nidhamu ni kitu muhimu sana katika mafanikio yoyote yale, na kwa namna hiyo tunajenga taifa ambalo baadae tutapata viongozi walio bora.
Bi. Maina ameahidi kufuatilia changamoto zilizotolewa na mkuu wa shule ikiwa ni pamoja na huduma ya maji safi kutoka kisima cha bonde la kwa Tom. Amesema atawasiliana na idara husika ili liweze kupatia ufumbuzi wa changamoto ya maji. Bi. Maina amesema bado wanaendelea kuomba walimu kutoka TAMISEMI ili kujaza nafasi zenye upungufu wa walimu. Amesema majengo yote chakavu katika shule ya sekondari Karatu yako katika Mpango wa kukarabatiwa.
walimu wa karatu sekondari wakiwa katika picha ya pamoja na meza kuu
Naye Mwenyekiti wa bodi ya shule sekondari Karatu Ndg. John Zakaria Tipee katika salamu zake kwa wanafunzi, amesema kuna wakati alikuwa anatembelea shule na kukuta ukimya. Lakini wanafunzi walikuwepo na walikuwa wanasoma, hiyo ni kuonesha namna wanafunzi walikuwa makini katika kutumia muda wao shuleni vizuri.
Amesema ilipotokea janga la ugonjwa wa corona alipata hofu kwamba wanafunzi watamalizaje maada zao darasani. Hasa ukizingati kwamba kuna wanafunzi wanatoka maeneo ya vijijini na hakuna mtandao au nyezo za kimawasiliano kama watu waliopo mjini. Amesema alipozungumza na walimu walimuambia wao tayari wamemaliza mada za masomo jambo ambalo lilimpa faraja.
Akitoa taarifa kwa mgeni rasmi Mkuu wa shule Ndg. Marko Anne amesema shule ya sekondari Karatu ilianza 1974 na ilianza ikiwa shule ya O-level. Amesema mwaka 1995 shule ilianza kuwa na kidato cha tano na walianza taasusi mbili lakini sasa shule ina taasusi kumi za kidato cha tano na sita.
Ndg. Anne amesema shule ilikuwa na watahiniwa 370 lakini kwa sababu mbalimbali watahiniwa wamebaki 366. Mtahiniwa mmoja ameenda kujisajili private na wengine watatu hawatafanya mtihani kwa sababu mbalimbali ikiwemo sababu za afya. Amesema wanafunzi waliandaliwa vizuri, hata wakati wanaondoka kutokana na janga la ugonjwa wa corona walipewa material ya kutosha ambayo yaliwasaidia kujisomea. Amesema mwaka jana wanafunzi waliopata daraja la kwanza walikuwa 91 na daraja la pili walikuwa 170 daraja la tatu 99 na daraja la nne wanafunzi 10. Amesema wanaomba Mungu wanafunzi wa mwaka huu wafanye vizuri zaidi kuliko mwaka jana.
wanafunzi wa karatu sekondari wakiwa katika picha pamoja na meza kuu
Wanafunzi nao wameeleza matarajio yao Ginde Laizer mwanafunzi wa Taasusi ya CBA na Rashidi Muzola Ramadhani mwanafunzi wa Taasusi PCB wamesema wamejianda vizuri, walikuwa wanasoma na walikuwa wanatumia wanafunzi wa kidato cha chini kuwalekeza ili yale waliyoyasoma yaendelee kukaa kichwani. Lakini walitumia muda wao katika kusali ili kuomba mungu awajalie waweze kufanya vizuri katika masomo yao ya kidato cha sita.
Wamesema wanafunzi waliopita kiwango chao cha ufaulu kimewapa ari ya wao kufanya vizuri zaidi ili waweze kuvunja rekodi. wamesema ikitokea wakapata matokeo ya chini zaidi ya kaka zao inamaana rekodi haitakuwa imevunjwa. Wao kama wanafunzi wamedhamira kuweka historia yao ili kuzidi kuipa heshima Karatu sekondari. wamesema wamejiandaa vizuri hata kipindi cha changamoto za janga la corona walikuwa wanaweza kutumia website ya shule kupata maswali na maandiko mbalimbali lakini pia kutumia vipindi vya television ya taifa TBC.
Mkuu wa shule ya sekondari Karatu kushoto mwalimu Marko Anne na Afisa elimu sekondari karatu Bi, Kalista Maina na Mwenyekiti wa Bodi ya shule ya sekondari Karatu Ndg. John Zakaria Tipee kulia wakiwa katika picha ya pamoja
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa