NA TEGEMEO KASTUS
Mkuu wa wilaya ya karatu Mh. Abbas Kayanda ameelekeza kukakamatwa kwa wanafunzi watatu, wanaosoma shule ya Msingi Matala na Njoro. Wanafunzi hao inadaiwa wamekataa kuendelea na shughuli za kimasomo ikidaiwa wanataka kuolewa.
Hayo yamesemwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Matala, malekezo hayo yametolewa baada ya wanafunzi hao kupata udhamini wa kusomeshwa na MO-Dweji. Mh. Kayanda amesema pamoja na wanafunzi hao kukamatwa ameelekeza kukamatwa kwa watu ambao wameshawishi mabinti hao, kutaka kuolewa. Amesema wazazi wa watoto hao wanaozuiwa watoto hao kusoma nao pia wakamatwe kwa sababu kumzuia mtoto wa shule kusoma ni dhuluma. Ameelekeza wazazi wanaohusika na watoto hao, baada ya kukamatwa kufikishwa mahakamani ili sheria zichukuliwe dhidi yao.
Mkuu wa wilaya ya Karatu, Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa Matala.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Waziri Mourice amesema katika shule ya Msingi Njoro na Matala kuna ufadhili wa Mohamedi Dweji kwa wanafunzi watatu ili kuwasaidia kuweza kusoma. Amesema baada ya kipindi cha mapuziko cha corona wanafunzi hao hawakurudi shuleni mpaka sasa. Amesema mmoja katika wale wawili wa Matala anafanyiwa mpango wa kuozeshwa. Ndg. Mourice amesema wazazi hao wamefanya makusudi kutowarudisha wanafunzi hao shuleni.
Sambamba na hilo Ndg. Mourice amesema ataleta mwalimu wa kike shule ya msingi Matala na watapeleka walimu wa kike shule ya msingi Njoro. Amesema wanafunzi wa kike wamekuwa wakipata shida sana hasa kupata mwalimu anayeweza kuwasikiliza na kuwalea wanafunzi wa kike.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Ndg. Waziri Mourice akieleza hali ya utoro wa wanafunzi katika Kijiji cha Matala.
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Matala Iddi Kiboko amesema changamoto kubwa wanayopata kwa wanafunzi wa Matala ni kutokuwa na mahudhurio mazuri darasani. Amesema wakati wanafunzi wanaposhindwa kuhudhuria darasani kwa siku tano zinazopangwa kwa juma zinafanya mwanafunzi kukosa baadhi ya vitu vinavyofundishwa darasani. Amesema hali hiyo ndiyo inayosababisha baadhi ya wanafunzi kufika darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika.
Amesema ili kusadia hali hiyo wazazi wanapaswa kuwasimamia wanafunzi wao kwa kuhakikisha wanakuwa wanamahudhurio mazuri shuleni. Mwalimu Kiboko amesema lazima wazazi pia wafuatilie maendeleo ya wanafunzi wao shuleni kwa kuhakikisha kazi za darasani wanazopewa zinafanyika, amesema ushirikiano wa mzazi na mwalimu ndio utakaosaidia kuinua kiwango cha ufaulu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa