Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa wilaya ya karatu. Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa mazingira bora na ulilenga kuhamasisha watu juu ya maboresho la daftari la wapiga kura zoezi linalotarajiwa kuanza kuanzia tarehe 18 july 2019.
Mhe.Theresia amesema Mkurugenzi wa wilaya ndiye Afisa mwandikishaji wa daftari la maboresho la wapiga kura. Amesema kama kuna mwanachi ambaye kitambulisho chake cha kura kimekatika au kimepotea ni vyema ajitokeze kwenye kituo cha maboresho ya daftari la mpiga kura. Amesema kama kuna mtu amehama kata, au eneo moja kwenda jingine wajitokeze kuboresha taarifa zao. Amesema usiporekebisha taarifa zako kama umehama kutoka eneo moja kwenda jingine utashindwa kupiga kura kwa diwani na mbunge na utakuwa na nafasi ya kupiga kura kwa raisi tu. Amesema zoezi la uandikishaji linafanyika mwaka huu, mwakani hakutakuwa na zoezi hilo la kuboresha taarifa la daftari la wapiga kura.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano uwanja wa Mazingira Bora.
Mhe. Theresia amesema kwa mwanachi ambaye hajahama au kupoteza kitambulisho chake hana haja ya kufanya marekebisho. Amesema vijana ambao watafikia umri wa miaka 18 mwakani mwezi wa kumi atapata nafasi ya kujiandikisha. Amewasihi sana vijana kujitokeza kwenye zoezi hilo, amesema hilo ndio kundi kubwa.Vituo vitafunguliwa kuanzia saa mbili kamili asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni na kutakuwa na matangazo mabalimbali yanayoelekeza juu ya zoezi hilo.
Mhe . Theresia amesema sifa ya mtu anayepaswa kuandikishwa kwenye daftari la maboresho ya kupiga ni mwananchi ambaye ni rai wa Tanzania. Amesema mtu anayepaswa kuandikishwa lazima awe ni rai wa Tanzania kwa kuzaliwa, kurithi au kuandikishwa. Kuandikishwa ni raia aliyekuwa hana uraia wa Tanzania na akaandikishwa na maafisa uhamiaji na kupata cheti cha uraia wa Tanzania. Amesema mwananchi huyo atapata fursa ya kujiandikisha na kupata kitambulisho cha kupiga kura. Ameongeza kusema kuna watu wanapata utanzania wa kurithi, huu unatokana na wazazi ambao wanaishi Tanzania lakini si watanzania wakapata mtoto. Mtoto anayezaliwa anapata haki ya utanzania kwa kurithi.
Mhe. Theresia amesema kuna watu ambao hawatapata nafasi ya kuandikishwa katika daftari la maboresho ya kupiga kura. Amesema mtu mwenye uraia wa nchi mbili, hatapata nafasi ya kuijiandikisha kwenye daftari la maboresho la wapiga kura. Amesema mtu ambaye ameshatumikia kifungo cha miezi 6 hataruhusiwa kujiandikisha. Amesema mtu aliyehukumiwa adhabu ya kifo au matatizo ya akili hawaruhusiwi kuandikishwa kwenye daftari la maboresho la wapiga kura. Mtu ambaye hajafikia umri wa miaka 18 naye hawezi kujiandikisha kwenye daftari la maboresho la wapiga kura.
Awali Afisa Mwandikishaji Ndugu Waziri Mourice amesema zoezi la kuandikisha watu waliopoteza kadi za mpiga kura, lazima waje na fomu za kudhibitisha upotevu wa kadi za kupiga kura. Zoezi hilo ni muhimu na linatarajia kuanza kuandikisha tarehe 18 mpaka tarehe 24 mwezi huu ambao ni muda wa siku 7. Ametoa wito watu kujitokeza kwa wakati badala ya kusubiri siku za mwisho za uandikishaji. Ndugu Waziri amesema zoezi hilo ni kielelezo cha namna serikali inavyofuata utawala bora. Amesema zoezi hilo ni muhimu sana na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kujiandikisha.
Ndugu Waziri amesema watatoa matangazo mfululizo kwa muda wa siku tatu wakati wa zoezi hilo. Amesema upande wa Karatu kuna vituo 11 vituo hivyo vitatambulishwa na kutangazwa kwa wananchi. Ndugu Waziri ametumia nafasi hiyo kuwatambulisha maafisa wasaidizi ngazi ya kata 14 kwa wananchi ili wawafahamu na kuwapa ushirikiano wakati wa zoezi la uandikishaji.
wananchi wakifuatilia Mkutano, Uwanja wa mazingira Bora
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa