Mkuu wa wilaya ya karatu Mhe. Theresia Mahongo, ametembelea na kuzungumza na waathirika wa mafuriko yaliyotokea kata ya Mang’ola. Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya.
Mhe. Mahongo ametembelea kijiji cha Langharerir ambacho waanachi 15 nyumba zao zimebomolewa na mvua zinazoendelea kunyesha. Malechand wananchi 30 nyumba zao zimeathirika na mafuriko ya maji ya mvua na Mang’ola barazani nyumba 44 zimebomoka kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. Mhe. Mahongo amewapa pole na ametoa wito kwa wananchi waliojenga na wanaoendelea kujenga nyumba katika mikondo ya maji kuondoka maeneo hayo, kwa sababu si maeneo salama. Amesisitiza wananchi kujenga nyumba za kudumu katika maeneo ambayo hakuna mikondo ya maji. Mhe. Mahongo amewataadharisha wananchi kwamba katika siku tano mfululizo mvua kubwa zinatarajiwa kunyesha amesema ni vyema watu wanao ishi mabondeni na kwenye mikondo ya maji kuchukua tahadhari na kuondoka maeneo hayo.
Mhe. Theresia Mahongo akimuhimiza mama Tumaini aliye Kushoto huko kijiji cha Langharer kuhama nyumba hiyo, iliyoharibika vibaya kama inavyoonekana nyuma ya picha.
Mhe. Mahongo amesema Malechand kuna drif ambalo limejengwa kwa mwinuko badala kuwa kwa mteremko ndio iliyochangia maji kufurika na kuingia kwenye makazi ya watu. Amesema drift hiyo itatabomolewa na utajengwa mfereji, amewapongeza wananchi wa Malechand kwa kuchukua tahadhari mapema. kuondoka maeneo yenye mafuriko na kutafuta makazi ya muda, Mhe. Mahongo amesema kwa sababu waathirika wameshatoka amelekeza uongozi wa Malechand kukaa kikao cha kijiji ili kuweka utaratibu wa waathirika kuweka makazi ya muda katika ofisi za maji.
Mhe Mahongo amesema pamoja na wananchi hao kukaaa katika eneo hilo la muda ametoa maelekezo ya viongozi wa kijiji kuweka katika maandishi mkataba na kuwapa waathirika hao ili waweze kukaa na kwa muda katika eneo hilo lilotengwa kwa makazi ya dharura. Lengo la kuandikisha ni kuepuka mkanganyiko siku za usoni juu ya namna walivyopewa idhini ya kuweka makazi ya Muda katika ofisi za maji zilizopo Malechand.
Mwenyekiti wa kijiji Malechand Marco Yoyo amesema kitendo cha kuwasiliana na wananchi wenzao walio nje ya Malechand kimewasaidia kuwapa taarifa mapema hivyo kunusuru athari za mafuriko. Ndugu Yoyo amesema kwa kushirikiana na Afisa tarafa walipiga la mbiu kuwapa tahadhari juu ya mafuriko. Amesema watu wasio na makazi walienda kujisitiri kwa ndugu jamaa na marafiki amesema hakuna mifugo iliyokwenda na maji.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa