Na Tegemeo Kastus
Wananchi wa kijiji cha Mikocheni kata ya Endamaghan wamefurahia kupata ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji. Halmashauri ya kijiji cha Mikocheni iandae utaratibu maalumu wa kuwatambua na kuwagawia wananchi wa kijiji cha Mikocheni ili waweze kujikita katika shughuli za kilimo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipofanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha mikocheni. Amesema utaratibu uliokuwa unafanywa na Halmashauri ya kijiji cha Mikocheni wa kumpa mwananchi mmoja hekari mia ili aweze kujenga visima vya maji vitatu ni batili. Amesema ameufuta mpango huo na amemuelekeza Afisa Mtendaji kata wa Endamaghan asimamie utaratibu wa kuwatambua na kuwagawia wananchi ardhi, ameongeza kusema ardhi ni mali. Ardhi haiongezeki lakini watu wanaongezeka, unaweza usiwe na uwezo wa kuiendeleza eneo leo lakini kesho ukapata uwezo wa kuliendeleza baaadae.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa Mikocheni.
Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda ameelekeza Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri pamoja na watu wa RUWASA kuchunguza fedha za iliyokuwa kamati ya maji Mikocheni na Endamaghan inayoitwa (Endamaiko) ili kujiridhisha na mapato na matumizi. Amesema hayo baada ya wananchi kulalamikia kukosekana kwa uwazi wa mapato na matumizi ya kamati hiyo ya maji.
Naye Afisa Mtendaji kata wa kijiji cha Mikocheni Ndg. Simon Mafie amesema kijiji cha Mikocheni huduma za maji safi na salama zimeathirika kutokana na miundo mbinu duni ya iliyowekwa na {Endamiko}. Amesema hata mradi wa maji wa shirika la world vision umeathirika kufanya kazi kwa sababu eneo walilojenga mashine za kusukumia maji safi na kusambaza kwa wananchi limekumbwa na mafuriko ya ziwa Eyasi.
Wananchi wakichangia katika mkutano huo wa hadhara Diwani mstaafu wa kata ya Endamaghan Mh. Sophia ameomba wakala wa barabara vijijini kujenga matoleo ya maji wanapokarabati barabara vijijini. Amesema kujenga barabara bila kuwa na matoleo ya maji kunasababisha maji kutuwama barabarani hivyo kuzidi kuharibu barabara.
Mkuu wa wilaya katika matukio tofauti akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mikocheni
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa