NA TEGEMEO KASTUS
Wananchi kujiunga na vikoba ni jambo jema kwasababu linawajengea wananchi uwezo wakuweka akiba ya fedha. Masharti yaliyopo kwenye taasisi za fedha yanafanya wananchi wengi kushindwa kukopesheka, lakini kikoba kinamuwezesha mwananchi aliye mwanakikundi kuweza kukopesheka katika kikundi chake.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu, mh. Abbas Kayanda wakati akizungumza na kikundi cha kikoba cha upendo kinachosimamiwa na Food for his children katika kijiji cha Endashang’wet kilichopo katika kata ya Daa.Amesema ili kuimarisha kikundi lazima kuwe na uaminifu katika utunzaji na urejeshaji wa fedha kwa wakati. Vikoba vikiwa imara baadae vikaunganishwa ndivyo vinaanzisha Saccos.
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ameomba wanakikundi wa upendo ambao wamekidhi vigezo kujiunga na mradi wa kopa mbuzi lipa mbuzi. Amesema ameutembelea na kuona mradi huo ni mradi wenye tija unalenga kuinua kipato cha familia duni. Watu waliojiunga na mradi huu maisha yao yamebadilika, wameimarika kiuchumi kwa kuweza kusomesha watoto mpaka chuo kikuuu lakini pia wamepata uwezo wa kujenga nyumba.
Mh. Abbas kayanda akizungumza na wanakikundi cha upendo katika ofisi ya kijiji cha Endashang'wet
Amesema mradi huu ni fursa kwa wananchi wa Karatu, wananchi wanapaswa kuwa na mtizamo chanya katika kupokea na kuutekeleza. Amesema ufugaji wa nyumbani bila kupeleka mifugo machungani ukisambaa kwa watu mbalimbali utasaidia kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji. Amesema ametembelea banda la mzee Emanuel Ramadhani ambaye amepandikiza mbuzi wa kisasa kwa mbuzi wa kienyeji na kupata vitoto vya mbuzi 11 vienye afya safi. Amesema mzee Ramadhani ambaye anaishi katika kitongoji cha chemchem kwa kupitia mradi huu wa mbuzi unaoendeshwa na Food for his children ameweza kulima jaruba za mbegu za vitungu (baruti) takriban vitalu 80.
Mh. Abbas kayanda akiwa katika banda la mzee Emmanuel Ramadhani
Bi, Honorina Honorati amesema kwa kutambua umuhimu wa afya za wafugaji mwaka huu wanatarajia kutoa bima ya afya kwa wananchi ambao ni wanachama wa shirika hilo ambalo si la serikali la Food for his children. Amesema lengo ni kujenga uelewa kwa wafugaji kujali na kutathimini afya zao. Amesema kwa mwaka ujao wafugaji ambao ni washirika wa food for his children watapaswa kuchangia sehemu ya bima hiyo ili kujenga uwezo wa kuthamini na kuchangia katika maswala ya maendeleo kwa jamii.
Amesema mradi huo unatarajiwa kufunguliwa katika kijiji cha Endashwang’weti Bi, Honorati ameshukuru serikali kwa ushrikiano mkubwa uliowezesha shirika la Food for his children kufanya kazi vizuri katika wilaya ya Karatu. Amesema shirika limekuwa likisadia katika sekta ya afya hasa katika kununua vitakasa mikono, na kununua vifaa vya kuchuruzisha maji ili kusaidia wananchi kujikinga na magonjwa ya mlipuko.
wanakikundi cha upendo wakiwa katika picha ya pamoja na Mh. Abbas Kayanda
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa