Na Tegemeo Kastus
Wanasheria vishoka wana wanawalagahi wananchi na kuwatoza gharama kubwa za fedha zisizo na msaada wowote wa kisheria. Wananchi wenye mashauri yao mahakamani wanapaswa kupata ushauri na msaaada wa kisheria kwa mawakili wanaotambulika kisheria.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda amesema hayo katika kilele cha siku ya sheria ya mawakili wanaotambulika na serikali kilichofanyika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya ya Karatu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 100 ya Mahakama kuu, katika kujenga nchi inayozingatia uhuru haki undugu amani na ustawi wa wananchi 1921- 2021. Amesema wananchi wanapaswa kuleta ushahidi na mashahidi ili shauri liamuliwe mahakamani kwa kuaangalia haki ipo wapi kwa mujibu wa sheria. Kuna kesi mbalimbali ambazo zimefunguliwa lakini hazitolewi ushahidi, mwisho wa siku kesi zinaenda kumalizwa nyumbani.
wananchi wakifuatailia matukio mbalimbali katika kilele cha siku ya sheria
Mh. Kayanda amesema baraza la ardhi na nyumba limekuwa na kesi nyingi za muda mrefu, ametoa rai kwa mwenyekiti wa baraza kuongeza kasi ya kusikiliza migogoro ya ardhi kwa maana kesi zinapochukuwa muda mrefu wananchi wanaanzaa kujenga tafsiri hasi juu ya kesi zao.
Ameomba wapelelezi kuongeza kasi ya uchunguzi wa kesi wanazopeleleza ili mashauri yakamilike mapema, amesema kumekuwa na malalamiko juu mahakama wanachi wakilalamika kuchelewa kupata nakala ya hukumu.
Mh Kayanda amesema wiki ya sheria ilifanyika katika uwanja wa mazingira bora, wiki hiyo ilikuwa maalumu kwa wananchi kupata msaada wa kisheria bure. Mwaka huu mwiitikio wa wananchi ulikuwa ni watu 120 ni mwamko mdogo mno. Ametoa rai kwa wananchi siku za usoni kujitokeza katika wiki ya sheria ili kupata msaada wa kisheria.
Akizungumza katika kilele cha sherehe za siku ya Mahakama Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama ya Karatu Mh. Is-haq Kuppa amesema mahakama imeanza kuendesha mashauri kwa mfumo wa Tehama. Amesema kesi zote zinasajiliwa kwa mfumo wa Tehama na imesaidia kupunguza kesi za nakala za hukumu.
Mh, Abbas Kayanda akiwa katika picha ya pamoja na mawakili
Mh. Kuppa amesema mahakama ya wilaya yaKaratu ina mashauri 122 amabyo yapo ambazo kituo ina mamlaka nazo ya kumaliza na kesi ambazo mashauri yanazuio, kesi ambazo hawana mamlaka nazo. Amesema mashauri hayo yamepungua na yako kwa uwiano wa kusikiliza kwa mahakimu watatu.
Mh. Kuppa amesema Karatu hakuna uhaba wa mawakili lakini wananchi wengi wanatumia wanasheria wasio rasmi. Amesema hii inasababisha haki za watu kupotea, kwa sababu mashauri yanakosa mashiko ya ushahidi unaotakiwa kisheria.
Mh, kuppa amesema kumekuwa na kasumba ya watu kufanya mauziano ya maeneo mkataba unaweka chini uthibitisho wa Mahakama. Mh kuppa amesema mahakama haifanyi uthibitisho wa mikataba, amesema hayo ni madhara ya kuandaa mikataba na watu ambo hawana weledi wa taaluma ya sheria.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa