Na Tegemeo Kastus
Mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna uhusiano na kuchukua( kunyang’anya) ardhi ya wananchi. Ni utaratibu wanaojiwekea wananchi wenyewe kupanga matumizi bora ya ardhi yao kutokana na shughuli za asili za eneo husika.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Theresia mahongo amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika kitongoji cha Gidamilanda katka kijiji cha Dumechang. Ameomba wananchi wa kitongoji hicho kutoa taarifa kwake moja kwa moja kwa mtu yeyote anayefanya upotoshaji dhidi ya mpango wa matumizi bora ya ardhi. Amesema watu wanaopotosha wanaturudisha nyuma badala ya kwenda mbele, mpango wa matumizi bora ya ardhi si wa afisa ardhi wala si mpango wa mkuu wa wilaya.
Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi umewekwa kwenye ilani ya chama cha mapinduzi kinachoongozwa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi. Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ulizinduliwa katika Mkoa wa manyara (babati) na waziri wa ardhi nyumba na makazi Mh. William Lukuvi.
Mpango wa matumizi bora ya ardhi unafanywa na wananchi wenyewe, amesema wananchi wataitishwa kwenye mkutano na watapanga matumizi ya ardhi katika eneo lao la kitongoji wao wenyewe. Mh. Mahongo amesema watu wanaongezeka lakini pia mifugo nayo inaongezeka, ukiangalia idadi ya watu waliopo kwenye kitongoji cha Gidamilanda kwa sasa si sawa na miaka ya nyuma amesema hata idadi ya mifugo pia inazidi kuongezeka. Amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ni kusaidia kutunza ardhi iliyopo ili iweze kutumika vizuri.
Amesema mpango huo unaweza kurekebishika amesema ikitokea kuna kitu cha ziada wananchi wanataka kiwe katika sehemu ya mpango wao wa ardhi, wanaitisha kikao wanajadiliana namna ya kuweka mipango yao vizuri. Ametoa onyo kwa watu watakao potosha mpango wa matumizi ya ardhi amesema hata wavumilia kabisa.
Awali katika mkutano huo katibu tawala wa wilaya ya karatu ndg, Abbas Kayanda alizungumza changamoto za kitongoji cha Gidamilanda; amesema kutokuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi kumesababisha watu kuendelea kuvamia maeneo kiholela. Amesema kuwa na matumizi bora ya ardhi kutasaidia kuepuka uvamizi wa meneo katika eneo hilo, wananchi sasa wanapaswa kushiriki kwenye mikutano ili kujadili namna ya kuweka ardhi katika mpango wa matumizi bora ya ardhi.Amesema hata matukio ya wageni wanaotoka pembezoni mwa wilaya nyingine na kuvamia eneo lao yatakwisha kabisa na wananchi wa Gidamilanda watatumia ardhi yao kwa matumizi watakayojipangia wao wenyewe .
wananchi wakiwa katika mkutano katika shule ya msingi Gidamilanda
Afisa ardhi wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Faraji Rushagama amesema mpango wa matumizi bora ya ardhi ni swala la kisheria ambalo linafanywa na wananchi wenyewe. Amesema mpango unahusisha shughuli za asili zinazofanywa katika eneo husika. Amesema mpango unasaidia kufahamu ni kipi kinafanywa na kijiji au kitongoji na kinafanyika kwa namna gani ?? ili kiweze kuboreshwa, amesema matumizi ya eneo husika na kiasi cha ardhi kinachopaswa kutumika kinapangwa na wananchi wenyewe wa eneo husika.
Amesema zoezi hilo wataalamu watajadiliana, kuelekezana na watashauriana na wakijiji au kitongoji kwa kina ameongeza kusema kama kuna mashaka na mtaalamu wa kupima wa wilaya na katika eneo husika kuna mtaalamu aliyesajiliwa na anatambulika basi atachukuliwa ili kusaidi zoezi la mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Ndg. Rushagama amesema sheria ya ardhi ya kijiji imewapa wananchi mamlaka ya kusimamia ardhi ya kijiji ambayo inahusika na kuilinda pamoja na kuipanga. Ameomba wananchi kutoa ushirikiano na kutunga sheria ndogo ambazo hazitatumika kuwaumiza wananchi wao wenyewe.
Nao wananchi wa kitongoji cha Gidamilanda wamesema namna walivyopokea swala la mpango bora wa matumizi bora ya ardhi katika eneo lao. Ndg. Dawte mkazi wa eneo hilo amesema awali walipata taarifa kwamba moja ya eneo lao ambalo linatumika kwa shughuli za malisho ya mifugo lingechukuliwa na kutegwa kwa ajili ya hifadhi ya game resereve. Kutokana na elimu waliyopata katika mkutano huo pamoja na ufafanuzi wa kina wa Mkuu wa wilaya kwamba hakuna eneo la kitongoji litakalochukuliwa, limewapa faraja wananchi wa Gidamilanda na mwitikio chanya juu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi.
wananchi wakifuatilia agenda za mkutano.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa