Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru kaya Masikini halmasahuri ya Karatu, mradi unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii -TASAF, wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia fedha za ruzuku ya mpango huo.
Wamesema kuwa fedha hizo zimewasaidia kumudu kupata mahitaji ya nyumbani ya familia, mahitaji ya watoto wa shule pamoja na kupata elimu ya ujasiriamali ya kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa fedha ambazo zimewapa mitaji ya kuanzisha miradi ya biashara ikiwemo kilimo na ufagaji.
Eladia Saruwat mkazi wa Rhotia, amekiri kunufaika na fedha hizo za ruzuku na zimemsaidia kukidhi mahitaji ya familia sambamba na kuwawezesha watoto wake kwenda shule wakiwa na mahitaji muhimu ya shule.
"Tunamshukuru rais wetu mama Samia, TASAF imetupa elimu ya ujasiriamali, tumeanzisha vikundi vya kuweka na kukopa, fedha ambazo zimetusaidia kupata mitaji na kuanzisha biashara ndogondogo" .Amesema Agatha.
Naye Marjat Kimolo amesema kuwa, TASAF imewawezesha kukuza mitaji yao kwenye kilimo na ufugaji, jambo ambalo limekuza uchumi wa kaya zao.
Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii - TASAF imetoa ruzuku ya shilingi milioni 134.6 kwa kaya 5,451 kwenye vijiji 61 vya Halmashauri hiyo ya Karatu ikiwa ni ruzuku ya mwezi Julai na Agosti, kwa mwaka wa fedha 2024/2025
Kaimu Mratibu wa TASAF Halmashauri ya Karatu Ndg. Atanas Sarwath, amekiri kupokea fedha hizo na tayari zoezi la malipo kwa kaya zilizo kwenye Mpango limeanza tarehe Novemba 04,2024 na litakamilika Novemba 10,2024.
"Tumepokea shilingi 134.6 kwa ajili ya kaya 5,451 ambapo kwa ajili ya ruzuku ya elimu na afya ambapo shilingi milioni 91.8 zitalipwa kwa fedha taslimu na Milioni 42. walengwa watalipwa kwa njia ya benki na mitandao ya simu".Amefafanua Kaimu Mratibu huyo.
Ameongeza kuwa fedha hizo zinawasaidi walengwa katika kujikimu na mahitaji ya familia ikiwemo chakula mahitaji ya shule kwa watoto, pamoja na kupata mitaji ya kuanzisha biashara ndogongo huku kaya zikiunda vikundi vya kuwekeza fedha na kukopeshana.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa