Wasimamizi watakao husika na mfumo wa usajili ICHF wamefanya semina ya siku mbili katika ukumbi wa Halmashauri. Semina hiyo imelenga kuwapa uwezo wa kufahamu mambo yanayohusu mfumo wa usajili wa ICHF iliyoboreshwa pamoja na kujifunza namna ya kutumia mfumo wa usajili.
Ndugu Emmanuel Carl muwezeshaji wa semina hiyo kwa wasimamizi (incharge) anasema, ICHF iliyoboreshwa inamwezesha mwananchi kupata matibabu kwa gharama nafuu. Semina hiyo ya ufahamu itasaidia wasimamizi hao kuhamasisha wananchi katika maeneo yao. Semina hiyo imetumika kuwawekea mfumo wa kutumia kwa njia ya simu ili kusajili watu katika ICHF. Pamoja na kuelekezwa namna za kutumia mfumo huo kwa ufasha ukihusisha Maafisa Tehama katika kutoa elimu.
Dkt Vicent Gyunda akitoa nasaha kwa wasimamizi
Ndugu Emmanuel amesema uhamasishaji ni vyema ukafanyika katika vikao vya kijiji, kata na Tarafa. Amesema kuna uhusiano mkubwa kati ya msimamizi wa ICHF na kituo kupata fedha nyingi kwa sababu ya uhamasishaji ya watu kutumia ICHF. Amesema ni lazima huduma iwe nzuri wakati wa mapokezi kwa wateja wa ICHF na sehemu ya dawa. Amesema utaratibu wa kutumia bima ya afya unaanza kwa kupata huduma zahanati na kama tatizo la ugonjwa nia kubwa unapewa hati kwenda kituo cha afya. Lakini kwa mteja aliyejiandikisha na ICHF aliyepata dharura mbali na eneo lake la makazi anaweza kupata matibabu katika kituo cha afya kilichopo karibu naye.
Ndugu Emammanuel amesema lengo ni kuwawezesha wananchi kutumia ICHF iliyoboreshwa na kuachana na mfumo wa kutoa malipo ya hapo kwa hapo. Upo muswada utakao pelekwa katika baraza la madiwani ili kupitisha na kuongeza fedha za malipo ya hapo kwa hapo. Ndugu Emmanul ameeleza namna fedha za ICHF zikavyowekwa kwenye account itayoandaliwa kwa ajili ya makusanyo kimkoa. Wilaya ya karatu ni moja ya wilaya za mwanzo katika mkoa wa Arusha kuanza kutumia bima ya ICHF.
Ndugu Emmanule muwezeshaji wa semina hiyo amewaasa wasimamizi wa mfuko huo wa bima ya afya iliyoboreshwa ICHF kufanya kazi kwa kujituma. Huduma bora zitawavutia watu wengi kujitokeza na kujiandikisha katika mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa. wawezeshaji hao wametoa vifaa mbalimbali kwa ajili matumizi ya mfumo wa ICHF ambavyo vimepokelewa na Kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Karatu.
Dkt. Vicent Gyunda Kaimu Mganga Mkuu amewapongeza wawezeshaji kwa kutoa semina hiyo elekezi kwa wasimamizi wa mfumo wa ICHF. Amewaomba wasimamizi wa ICHF iliyoboreshwa kufanyia kazi kwa vitendo mafunzo waliyopata. Amesema wasimamizi ni vyema wakaonesha ueledi katika utendaji wao kwa kuhamasisha wananchi wengi kujiandikisha katika mfuko wa ICHF iliyoboreshwa.
Wasimamizi wakifuatailia semina ka umakini.
Wasimamizi katika matukio mbalimbali kwenye semina.
Wasimamizi katika Matukio mbalimbli wakati wa semina.
Dkt. Vicent akipokea vifaa kwa wawezeshaji wa semina ya ICHF
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa