Zikiwa zimesalia Siku tatu Kuelekea simu maalumu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024, Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura pamoja na wasimamizi wa vijiji wamepatiwa mafunzo pamoja na Kuapishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.
Kupitia Semina hiyo wasimamizi hao wamepatiwa mafunzo namna ya kuratibu na kufanikisha zoezi laupigaji kura, kuhesabu kura pamoja na kutangaza Matokeo ya uchaguzi katika vituo vyao husika.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika tarehe 27 November 2024 siku ya Jumatano hivyo wananchi wote wanaasisitizwa kujitokeza kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotajwa kuwa uchaguzi Muhimu kwa kila Mwananchi.
“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa