NA TEGEMEO KASTUS
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi mkuu ngazi ya kata unaotarajiwa kufanyika 28/10/2020 wapatao 28 wameapa mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Mh. I. Kuppa. Uteuzi wa wasimamizi wasaidizi umeanza rasmi tarehe 5 mwezi wa nane 2020.
Hayo yamesemwa na Msimamizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya Ndg. Waziri Mourice wakati akizindua mafunzo ya siku tatu ya wasimamizi wa uchaguzi kwa ngazi ya kata. Ndg. Mourice amesema kila kata itakuwa na wasimamizi wasaidizi wawili.amesema kiapo hicho kinamaanisha wateule hao wamekuwa watumishi wa tume ya taifa ya uchaguzi licha kuwa na majukumu mengine, bado watakuwa wanafanya kazi kama watumishi.
Picha za matukio ofauti wakati wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi wakiwa wanaapa
Ndg. Mourice amesema kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata wanatakiwa kutoa taarifa kwa kila jambo wanalolifanya linalohusiana na uchaguzi kwa msimamizi wa uchaguzi wa jimbo au wasimamizi wasaidizi wa jimbo. Ameongeza kusema mambo yote yanayofanywa kuhusiana na uchaguzi hayatolewi ufafanuzi na wasimamizi wasaidizi wa kata, amesema maswala ya uchaguzi yanatolewa taarifa na msimamizi wa uchaguzi wa ngazi ya jimbo au Msimamizi msaidizi wa ngazi ya jimbo au mtu atakayechaguliwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo.
Ndg. Waziri Mourice Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Karatu akifungua semina ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata
Ndg. Waziri Mourice amesema kwa mujibu wakifungu cha 126 cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura ya 343 tume imepewa mamlaka ya kuandaa maelekezo mbalimbali kwa ajili ya watendaji wa uchaguzi ili kuwezesha utekelezaji bora wa majukumu yao. Kwa mujibu wa kifungu cha 7 sehemu ya pili cha sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343 kifungu cha tisa sehemu ya pili ya sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa sura ya 292 tume inaweza kuteuwa kwa nyadhifa au kwa majina msimamizi msaidizi wa uchaguzi kwa jimbo au kata kwa idadi itakayoona inafaa.
Ndg. Mourice amesema sifa kubwa ni kuwa mtumishi wa umma amesema kuna baadhi ya majimbo kwenye nchi yetu wasimamizi wa uchaguzi si wakurugenzi. Kuwa mkurugenzi wa Halmashauri si sifa pekee kuwa msimamizi wa uchaguzi, amesema tume ya taifa ya uchaguzi imepewa mamlaka ya kumteuwa mtu yeyeto kwa ngazi ya jimbo au kata. Amesema wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi watatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; sheria ya taifa ya uchaguzi sura 343 sheria ya gharama za uchaguzi sura 278 kanuni za uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani za mwaka 2020.
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi mkuu wa ngazi ya wakiapa
Amesema wasimamizi wasaidizi wanatakiwa kufuata muongozo wa utoaji elimu ya mpiga kura na maadili ya uchaguzi ya mwaka 2020 pamoja na maelekezo mengine yatakayotolewa na tume ya taifa ya uchaguzi. Ndg. Mourice amewapongeza walioteuliwa amesema ni vyema wakazingatia mafunzo hayo ya siku tatu yanayofanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa