Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Karatu leo. Katika ziara yake amekutana na Watendaji wa Halmashauri, Makatibu Tarafa na Watendaji Kata katika ukumbi wa KDA Wilayani Karatu.
Mhe. Gambo amewaelekeza watendaji kusimamia wananchi kulipa kodi ya majengo; amesema watendaji wa kata, watendaji ngazi ya kijiji na kitongoji kutambua idadi ya nyumba zilizopo katika maeneo yao na kuhakikisha nyumba hizo zinalipiwa kodi ya majengo. Kodi ya majengo inalipwa kwa kuangalia hati ya umiliki wa nyumba, na inatakiwa kulipwa kila mwaka. Mwisho wa kulipia kodi hiyo ya majengo kwa mwaka huu ni tarehe 30 Mwezi wa sita.
Mhe. Gambo amewaelekeza watendaji wa kijiji na kata kuja na mpango mkakati kuondoa changamoto ya madarasa kwa wanafunzi wa shule za msingi na awali katika kipindi cha mwezi wa tatu mpaka wa kumi. Mhe. Gambo amehimiza watendaji kuendelea kufuatilia wazazi ambao wamezembea kupeleka watoto shule, hasa watoto ambao wanapaswa kuandikishwa darasa la kwanza na elimu ya awali. Pia amewaelekeza watendaji kutoa mchanganuo wa wanafunzi 659 waliofaulu kwenda sekondari na hawajaripoti. Lengo likiwa ni kuwawajibisha wazazi walioshindwa kuwapeleka wanafunzi shule kwa sababu za utoro.
Mhe. Gambo amemkabidhi Mkuu wa wilaya ya Karatu viatambulisho vingine elfu kumi na mbili vya wafanyabiashara wadogo. Amesema mtu yeyote atakayekwamisha au kupotosha zoezi hili atakamatwa na kupelekwa mahakamani. Mhe, Gambo amewaelekeza watendaji kuondoa urasimu katika utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogo.
Awali Halmashauri ya Karatu walipata vitambulisho elfu tatu na sasa wamepata vitambulisho vingine elfu kumi na mbili. Dhamira ya serikali ya kutoa vitambulisho ni kuwaondolea usumbufu ambao wamekuwa wakiupata wafanya biashara wadogo. Mhe. Gambo amesema kitambulisho kinatolewa kwa sekta ambayo siyo rasmi ili wajasiriamali hao waweze kutambuliwa. Serikali inataka wafanyabishara hao wadogo waweze kukua na kulipa kodi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa