Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe.Theresia Mahongo amefungua kikao cha wadau wa afya katika kitengo kinachohusiana na maswala ya lishe. Kikao cha wadau wa lishe kilienga kuendelea kujenga elimu ya ufahamu kwa wananchi pamoja na watendaji kata wa wilaya ya Karatu kusaini mkataba wa utekelezaji na uboreshaji wa elimu lishe.
Mhe. Theresia amesema zamani kulikuwa na utaratibu kwa mama mtarajiwa kupewa mafunzo kwanza kabla ya kupata chanjo na kupata elimu ya kuandaa chakula cha mtoto. Amesema elimu haina mwisho amehimiza wakufunzi wa afya kuendelea kutoa elimu kwa wakinamama wajawazito. Amesema mama mjamzito anapaswa kuzingatia kula vyakula vienye lishe bora,wanga mafuta na protini. Kuzingatia kula vyakula vienye vitamin na kukamilisha mahudhurio yote manne ya kiliniki kama wataalamu watakavyoelekeza. Mhe Theresia ametoa wito kwa wakinamama kufuata maelekezo ya kitaalamu ya kunyonyesha watoto, amesema maziwa ya mama kwa mtoto ni muhimu kwa sababu yana virutubisho vyote.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amesema atakuwa anataka ripoti ya watendaji kila eneo atakalofanya ziara ili kuona nini kumefanyika !! Mhe. Theresia amesema lazima kila mtendaji awe na mpango kazi ili waweze kutimiza malengo. Amesema sawa katika mpango kazi kuna wakati dharura zinatokea katika kazi lakini bado mpango kazi ni kitu muhimu katika uwajibikaji wa kila siku. Ameomba watendaji kujipanga katika utendaji wa kazi ili kuleta mfanikio chanya.
Dkt. Mustafa Waziri Mganga Mkuu wa Wilaya ya Karatu.
Awali katika taarifa yake Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Mustafa Waziri amesema moja ya mafanikio katika swala la lishe ni kuunda kamati ya lishe ya wilaya. Mwaka huu wa fedha tumetenga kiasi cha shilling million 48 ambayo itajikita katika shughuli za lishe kwa wilaya nzima. Dkt Mustafa mesema wameweza kutoa chanjo ya vitamin A na dawa za minyoo kwa 100%. Amesema idara inaendelea na jitihada za matibabu ya utapiamlo mkali na kuongeza kiwango cha utoaji elimu ya lishe kwa jamii.
Dkt Mustafa amesema Halmashauri inaingia mikataba wa AFUA na maafisa watendaji wa kata ili nao waipeleke kwa maafisa watendaji wa ngazi ya kijiji ikiwa ni moja ya njia ya kuboresha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika kata, vijiji pamoja na mitaa. Amesema mikataba hiyo ni agizo la waziri wa tamisemi ambayo aliagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kuingia mikataba ya AFUA na watendaji kata zote katika Halmashauri zote. Agizo hilo la waziri wa tamisemi lilitolewa katika sherehe za mradi wa lishe endelevu mkoani Rukwa, malengo ya mikataba hiyo ni sawa na ile iliyosainiwa na waziri wa nchi ofisi ya rais Tamisemi na wakuu wa mikoa yote Tanzania bara 19/12/2017. Agizo lilianza kutumika kuanzia 1/1/2018 ili kufanikisha hali ya lishe na kupunguza athari za utapiamlo katika kata, vijiji na mitaa. Dkt. Mustafa amesema Utekelezaji wa agizo hilo kwa watendaji kata umeanza kutekelezwa kuanzia 1/7/2019
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa