NA TEGEMEO KASTUS
Muundo wa kipindi cha pili cha awamu ya tatu ya Tasaf umeazingatia mapungufu yaliyotokea katika kipindi cha kwanza kwa kufanya maboresho zaidi. Semina ya uelimishaji ilenge kutoa uelewa mzuri wa namna ambavyo walenga wanapatikana ili kuondoa malalamiko katika jamii. Ili kusaidia kupata uelewa wa pamoja wa viongozi na watendaji itakapofika wakati wa utambuzi wa walengwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas kayanda wakati akizindua kikao kazi cha kujenga uelewa kwa wadau kuhusu mpango wa Tasaf kipindi cha pili ya awamu ya tatu. Amesema utekelezaji wa shughuli za Tasaf ni moja ya nyenzo za kupambana na umaskini. Zaidi ya kaya million moja zimewezeshwa na Tasaf katika kupambana na umaskini. Amesema watendaji watapimwa kwa kuangalia mafanikio ya walengwa, ameongeza kusema viongozi wanapaswa kuhamasisha ili kusaidia kupata taarifa sahihi za walengwa kwenye maeneo yao wakati wa utambuzi.
Watendaji wakifuatilia kwa makini hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi
Mh. Kayanda amesema fedha za ruzuku zinazotolewa na Tasaf zimesaidia kuboresha maisha ya walengwa, amesema kuna walenga ambao wameanzisha shughuli za ufugaji, wamejenga nyumba na kufanikiwa kuanzisha biashara. Lakini hata hivyo bado kuna walenga ambao hawajabadilisha hali ya maisha yao, ameelekeza watendaji kuwapa ushauri na maarifa ya kina ili walengwa waweze kujihusisha katika shughuli ambazo zitajenga uwezo wa kuinua kipato chao.
Akizungumza kuhusu changamoto Mh. Kayanda amesema kuna changamoto ya watu ambao hawana sifa za kuingia kuwa walengwa lakini wanaingia kwa utashi wa watu binafsi. Ametoa rai kwa watendaji kutenda haki na kuhakikisha wanafanya usajili wa watu wenye sifa bila kufanya upendeleo ili kukamilisha zoezi la uandikishaji kikamilifu.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. John Lucian amesema waratibu wa Tasaf wamekuwa wanafanya kazi nzuri sana katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Tasaf wamefanya kazi nzuri na mafanikio ni makubwa, amesema kuna miundo mbinu imejengwa kwa fedha za Tasaf katika kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii lakini bado thamani ya fedha kwenye miradi, inaonekana na inaendana na thamani ya miundo mbinu iliyojengwa.
Mh. Luciana amesema changamoto zipo haziwezi kukosekana mathalani kwenye mikutano mikuu ya kijiji kuna baadhi ya walengwa wanaochaguliwa kwa ushabiki. Ameomba viongozi kusimama imara na kufanya ufuatiliaji wa kina ili wenye sifa stahiki waweze kutambuliwa. Amekemea tabia ya baadhi ya walengwa wanaofanya matumizi mabaya ya fedha kwa kutumia kwa ajili ya ulevi, amesema hilo ni jambo la aibu tunapaswa viongozi tusimame katika nafasi zetu na kukemea tabia hizo zinazoleta taswira mbaya.
Picha katika matukio wakati wa kikao kazi
Awali katika taarifa iliyosomwa na muwakilishi wa tasaf kutoka makao makuu na Ndg. Peter Lwanda amaesema tathimini ya kwanza katika kipindi cha kwanza awamu ya tatu ya Tasaf imeonesha umaskini kwa kaya za walenga katika kupata mahitaji muhimu umepungua kwa 10% na umaskini uliokithiri kwa kaya za walengwa umepungua kwa 12% . Amesema katika kipindi cha kwanza Tasaf haikufika katika maeneo yote lakini kwa wamu hii ya kipindi cha pili cha awamu ya tatu itafika kila maeneo yote ambayo hayakuwahi kufikiwa na Tasaf.
matukio katika picha wakati wa kikao kazi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa