NA TEGEMEO KASTUS
Watendaji wa vijiji na kata waaswa kuwa waadilifu na mienendo mizuri katika utendaji wa kazi na kuishi katika maadili utumishi wa umma. Watendaji wa kijiji na kata ndio kioo cha watumishi wa chini mnaowasimamia kwenye ngazi ya kijiji na ngazi ya kata. Lazima mjikite katika kusimamia taarifa za mapato na matumizi na kuhakikisha zinasomwa kwa wakati ili kujengwa taswira ya uwazi.
Hayo yamejiri katika kikao cha Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda na Watendaji kata na vijiji wote wa wilaya ya Karatu kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri. Amesema kuna watendaji wa vijiji ambao hawajaandika na kusoma taarifa za mapato na matumizi tangu mwaka 2019. Hali hiyo inaleta mashaka katika utendaji wa kazi wa kila siku katika maeneo yao ya kiutawala.
Watendaji wakiwa katika kikao kwenye ukumbi wa Halmashauri
Mh. Kayanda amesema kuna vijiji vinaongoza kwa kuwa na mapato makubwa, lakini hakuna utaratibu wa kukusanya ushuru kwa kutumia (pos) mfumo wa kieletronic. Amesema haya ni mambo ambayo yanapaswa kufanywa na kusimamiwa na watendaji kama miongozo ya serikali inavyoelekeza.
Mh. Kayanda amesema kuna baadhi ya watendaji wa kijiji hawasikilizi na kufuata maelekezo wanayoelekezwa na watendaji wa kata. Amesema jambo hilo sio sahihi, mtendaji wa kata ni msimamizi wa shughuli zote za serikali katika ngazi ya kata. Mh. Kayanda amekemea tabia nyingine ya watendaji wanaohama kutoka eneo moja kwenda jingine lakini bado anafanya kazi za kituo cha awali bila kukabidhi ofisi, amesema tabia hizo sio nzuri zinaleta usumbufu kwa wananchi wanaohitaji huduma.
picha katika matukio wakati wa kikao cha watendaji wa kijiji na kata
Mh. Kayanda amesema Ofisi za serikali zinapaswa kufanya kazi wakati wote amesema kuna tabia ya za watendaji kutokuwepo katika vituo vya kazi siku za jumamosi na jumapili. Amesema kufanya hivyo kunawanyima wananchi kupata huduma; watendaji wanapaswa kutembelea taasisi zilizo katika maeneo yao na kujua mwenendo wa taasisi hizo, pamoja na kutafuta ufumbuzi wa kero na malalamiko ya wananchi katika maeneo yao ya kiutawala.
Mh.Kayanda amesema jukumu la watendaji ni kutoa elimu na kuhamasisha wananchi katika shughuli za kujiletea maendeleo. Amesema watendaji wanapaswa kusimamia kesi za utoro wa wanafunzi shuleni, kusimamia kesi za mimba shuleni ili kudhibiti vitendo hivyo vinavyozorotesha maendeleo ya elimu. Ameongeza kusema mtendaji anapaswa kuhamasisha wananchi juu ya kujiunga na mfuko wa bima ya afya ambayo uandikishaji wake kwa wilaya ya Karatu bado upo chini. Ameongeza kusema watendaji wanapaswa kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa kuwa na vitambulisho vya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo, ambao kwa sasa, Mjasiriamali atalipia mwenyewe kwenye control number na baadae Afisa biashara wa wilaya atathibitisha na kutoa kitambulisho.
matukio katika picha wakati wa kikao
Akizungumzia swala la vitambulisho vya mwaka jana Mh. Kayanda amesema kuna kiasi cha million tatu na elfu themanini za mwaka jana ambazo zimepotea kwa njia ya udanganyifu. Ametoa wito kwa watendaji kuhakikisha kiasi hicho cha fedha kinarejeshwa. Kiasi hicho cha fedha ni malipo ya vitambulisho vya ujasiriamali ambavyo stakabadhi zake zilikaguliwa na mamlaka ya mapato Tanzania (Tra) na kubainika zilikuwa ni stabakadhi feki. Katika malipo hayo ya vitambulisho vya ujasiriamali kuna kata ambazo hazikukutwa na changamoto stakakabadhi feki ambazo ni kata ya Buger, kata ya Mbulumbulu kata ya Baray na kata ya Endamarariek.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa