NA TEGEMEO KASTUS
Lazima tuongeze juhudi katika kusimamia ukusanyaji wa mapato ili tuweze kuendelea kujenga miradi ya maendeleo. Kuna wafanyabiashara wanabiashara zaidi ya moja lakini wanaleseni moja ya biashara. Sambamba na leseni lazima tuongeze ufuatiliaji na usimamiaji wa ushuru wa huduma ili tuweze kutimiza malengo tuliojiwekea.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika kikao kazi na watendaji wa Mamlaka ya mji mdogo uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Amesema kuna ulegevu katika ukusanyaji wa mapato kwa watendaji, lazima watendaji wa mamlaka waongeze ubunifu katika kuongeza vyanzo vingine vya mapato ili kuongeza na kuimarisha ukusanyaji wa mapato kama ilivyopitishwa na bajeti ya Halmashauri.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na watendaji wa mji mdogo Karatu.
Amesema watendaji wa mji mdogo wanapaswa kusimamia usafi wa mazingira katika eneo la mamlaka ya mji mdogo. Hali ya usafi wa mazingira bado hairidhishi, Mh Kayanda amesema watendaji wa mji mdogo waweke mipango mkakati wa kusimamia usafi wa mazingira na kudhibiti tabia za utupaji wa uchafu hovyo, ikiwa ni pamoja na kuweka siku moja kwa ajili ya usafi wa mazingira ili kila mwananchi ajishughulishe na usafi katika eneo lake analoishi.
Watendaji wa mji mdogo katika kikao kazi
Kuhusu usimamizi wa miradi ya maendeleo Mh. Kayanda amesema watendaji wa mji mdogo wanapaswa kufuatilia na kushirikiana na watendaji wa Halmashauri katika kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao. Mh. Kayanda amepongeza jitihada za diwani wa Ganako kwa jitihada zake zakusimamia ujenzi katika zahanati ya Sumawe. Amesema viongozi wa maeneo husika wakifahamu ujenzi wa miradi ya maendeleo inasaidia kujua uhalisia wa mradi wenyewe na inaondoa mianya ya udanganyifu. Ametoa rai kwa viongozi wa mji mdogo kuepuka matumizi mabaya ya madaraka na badala yake waongoze wananchi katika utashi wa kutenda matendo mema.
Akizungumzia hali ya ulinzi na usalama Mh. Kayanda ametoa wito kwa watendaji wa mji mdogo kutoa taarifa za uhalifu kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Ameongeza kusema kumekuwa na vitendo vya udokozi katika makazi yetu tunayoishi lakini utoaji wa taarifa za vitendo vya uhalifu umekuwa mdogo. Amesema jukumu la ulinzi na usalama katika makazi yetu ni jukumu la kila raia mwema na sio kwa vyombo vya ulinzi na usalama pekee. Amesema ili kuimarisha ulinzi na usalama ni vyema watendaji wa mji mdogo waanzishe ulinzi shirikishi katika maeneo ya kiutendaji.
Matukio katika picha wakati wakikao cha watendaji wa mji mdogo na mkuu wa wilaya ya Karatu.
Kuhusu usikilizaji wa kero za wananchi, Mh, Kayanda amesema watendaji watenge siku moja kwa ajili ya kutatua kero za wananchi. Amesema hakuna jambo la faraja kwa mwanachi kama kiongozi kusikiliza kero na kutoa njia sahihi za utatuzi wa chamgamoto zinazomkabili. Amesema changamoto za migogoro ya ardhi ni vyema zikapaelekwa katika baraza la ardhi, changamoto za matunzo ya watoto zipelekwe ustawi wa jamii. Amesema viongozi wanapaswa kuwa wasuluhishi wa migogoro inayotokea kwenye jamii.
Akizungumzia kuhusu swala la kuwa na mamlaka ya mji mdogo kamili mh. Kayanda amesema lazima watendaji wa mji mdogo wafanye tathimini ya vigezo vinavyotakiwa ili waweze kutimiza. Amesema watendaji wa mji mdogo wanapaswa kuwa na mkakati maalumu wa kutimizia vigezo hivyo vya mamlaka ya mji mdogo. Mh. Kayanda amesema anadhamira ya dhati ya kuona siku moja karatu inapata mamlaa kamili ya mji mdogo. Amesema tukipata mamlaka kamili ya mji mdogo kamili itasaidia kuchochea maendeleo ya wilaya ya karatu na itasaidia kupata bajeti mbili katika wilaya moja.
Matukio katika picha wakati wa kikao kazi cha mamlaka ya mji mdogo Karatu.
kuhusu mafanikio mabalimbali ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, amesema lazima watendaji wazungumze yaliyotekelezwa katika Halamshauri ya wilaya ya Karatu, Mh Kayanda amesema kua kiasi cha billion 1 ambacho kimetolewa na serikali kupitia wakala wa barabara mjini na vijijini kwa ajili ya kufungua barabara mbalimbali zilizokuwa zimefungwa. Amesema pamoja na kuelezea miradi ya mendeleo iliyofanya na serikali lazima pia tushirikishe wananchi katika usomwaji wa mapato na matumizi katika maeneo yetu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa