Kikao cha baraza la madiwani kimeendelea kwa siku ya pili leo, na kimejadili taarifa mbalimbali za kamati. Kikao kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Jublate Mnyenye.
Baraza limejadili taarifa iliyotoa mapendekezo ya kufidiwa ardhi wananchi waliokuwa wanadai, ili kumaliza baadhi ya migogoro ya ardhi na kuwezesha uendelezaji wa maeneo husika kwa matumizi yaliyopangwa.Wadai sita waliopitishiwa na kukubaliwa na vikao mbalimbali vya Halmashauri kwa ajili ya kufidiwa, ni Ndugu Benedicto Modaha ambaye kiwanja chake na .67 kitalu ‘k’ Karatu mjini kiliathiriwa na ujenzi / upanuzi wa kituo cha afya Karatu mjini. Ndugu James Paulo kiwanja chake na, 195 kitalu ‘J’ Karatu mjini kiwanja kiligawiwa mara mbili kimakosa. Bi Anastazia Bruno mwenye kiwanja na. 323 kitalu ‘J’ Karatu Mjini kiwanja kiligawiwa mara mbili kimakosa. Ndugu Paskali Sighis mwenye kiwanja na. 85 kitalu ‘G’ Karatu mjini kiwanja kiliathiriwa na upomaji mwaka 2000 na hakufidiwa. Ndugu Halfa Karonga mwenye kiwanja na.’ G’kambi ya fisi eneo lake lilipitishwa barabara wakati wa upimaji wa awali wa eneo hilo. Ndugu Baran Akonay mwenye kiwanja na. 137 ‘F’ kiwanja killigawiwa mara mbili kimakosa.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo ametoa maelekezo kwa baraza la madiwani kuchukua hatua kali kwa watendaji waliosababisha wananchi kupewa viwanja mara mbili. Amesema kufanya double allocation ni kosa kubwa sana, ameomba madiwani waiamini kamati ili wanachi wapewe fidia haraka.
Mhe. Theresia ameipongeza Halmashauri ya Karatu kwa kupata hati safi, amesema Halmashauri inaboreka katika utunzaji wa hesabu za serikali. Ameomba watendaji kuondoa hoja za kimfumo ambazo hazitekelezeki. Mhe. Theresia amesikitika kuona wawekezaji waliomba kuwekeza kwenye uwanja wa michezo wa Endoro na chuo cha michezo tangu mwezi wanne mwaka jana lakini wakanyimwa ushirikiano na watendaji. Uwekezaji katika michezo ni fursa ya kiuchumi amehimiza watendaji kushughulikia swala hilo mara moja.
Mhe. Theresia amehimiza baraza kuongeza mapato ya Halmashauri; amesema kiwanda cha maziwa ambacho kimelala, kinauhitaji wa shilingi million thelathini, ameelekeza baraza la madiwani kuliangalia swala hilo kwa upekee. Kiwanda hicho kikiendelea na uzalishaji kitatoa fursa za ajira, amesema kuna kiwanda cha unga jengo limekamilika tangu mwaka jana. Swala kuendeleza kiwanda cha unga si lazima fedha zitoke kwenye bajeti ya Halmashauri kama Halmashauri haina uwezo ingie ubia na wawekezaji ili kiwanda kianze uzalishaji.
Waheshimiwa madiwani katika kikao cha baraza la madiwani.
Mhe. Jublate Mnyenye Mwenyekiti wa Halmashauri akiendesha kikao cha baraza la madiwani.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa