• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WATENDAJI WATEKELEZA MAELEKEZO KIKAMILIFU

Posted on: August 24th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Jengo la choo cha mnadani lilokuwa limetelekezwa kwa muda mrefu, na miunndo mbinu yake kuharibiwa limekarabatiwa upya. Ukarabati wa maliwato umefanyika baada ya Mkuu wa wilaya kukagua na kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hlamshauri ya Karatu kukarabati na kuweka walinzi ili wafanyabiashara wapate huduma za maliwato.

Hayo yamebainika baada ya Mkuu wa wilaya a Karatu Mh.Abbas Kayanda pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kufanya ukaguzi katika jengo hilo lilopo katika eneo la mnadani Karatu. Ukarabati wa jengo hilo utasaidia wafanyabishara kupata huduma ya maliwato bila kufanya uchafuzi wa mazingira.

Hali ya Jengo la  Maliwato jinsi ilivyo sasa baada ya ukarabati mkubwa kufanyika eneo la Mnadani Karatu.

Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ujenzi wa zahanati  wa zahanati ya Ngaibara  na ametoa maelekezo  Mahususi kwa watendaji kuhakikisha ujenzi miundo mbinu ya majengo unakamilika haraka iwezekanavyo. Wakti huo huo  Mh. Kayanda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa jamvi katika jengo la maabara unaofanyika kituo cha afya Endabash baada ya kutembelea eneo la ujenzi.

Mh. Abbas Kayanda akikagua mashine mpya zilizoletwa katika kituo cha afya Endabash.

Mh. Kayanda amejionea vifaa vipya vilivyoletwa na Msd kwa katika Kituo cha afya Endabash ikiwemo mashine ya kutunzia watoto wachanga (incubator)   mashine kwa ajili ya wagonjwa wa pumu inayosaidia mgonjwa wa pumu kuvuta na kurudi katika hali ya kawaida. Mashine Maalum kwa ajili ya kuchemshia vifaa vya hospitali, kuepusha maambukizi kwa kutumia vifaa lakini pia kuna mashine ya kupimia kipimo kikubwa cha damu.

Mh. Abbas Kayanda akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya daraja la barabara.

Mh. Kayanda ametembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mnadani Endabash kuelekea Endamarariek  pamoja na ujenzi wa Josho. Miradi yote iliyotembelewa iko katika hali nzuri na ametoa rai kwa viongozi kuzuia kupitisha ngombe kwenye barabara ili kuepusha uharibifu wa barabara. Ameelekeza uongozi wa kijiji kusimamia  usafi na kulitunza jengo la mradi wa machinjio ya mnadani Endabash.

Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ujenzi wa  mradi wa maji kitongoji cha Kansay mradi ambao utasaidia shule ya msingi Haraa kupata maji pamoja na kusambaza huduma ya maji kwa wananchi. Sambamba na mradi huo ametembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa maji shule ya msingi Geer ambao umeanza kufanya kazi na kusaidia shule na  wanakijiji wa eneo hilo.

Mh. Abbas Kayanda akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya Machinjio Mnadani Endabash.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MILIONI 400 ZATOLEWA KARATU, KUJENGA MABWENI NA MADARASA EYASI SEKONDARI

    January 30, 2025
  • WASIMAMIZI WAASWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024.

    November 23, 2024
  • JESHI LA AKIBA MKAWE WAZALENDO KWA TAIFA

    November 23, 2024
  • HALMASHAURI YAZINDUA KITABU CHA MPANGO MKAKATI WA UKUSANYAJI MAPATO.

    November 19, 2024
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa