Maadhimisho ya siku ya mtoto wa mtaani duniani ambayo yameenda sambamba na kupinga ukatili, yamefanyika leo kwa maandamano ya amani. Watoto wameandamana wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti tofauti wa kupinga unyanyasaji kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Karatu na kuelekea Uwanja wa Mazingira Bora.
Maadhimisho ya mtoto wa mtaani yalikuwa na kauli mbiu ya”zingatia usawa, funguka usalama wake wajibu wangu”. Ndugu. Felix Sulle Afisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Karatu mbaye amemuwakilisha mgeni rasmi amesema ujumbe huo ni mzito. Amesema watoto wanahaki ya kusoma, kulindwa, kusikilizwa na kushirikishwa. Amesema kuna sheria ya mtoto ya mwaka 2009, ambayo hairuhusu mtoto kufanyiwa vitendo viovu. Watoto wanapaswa kufahamu sheria hii ili waweze kupigania haki zao. Ndugu. Sulle ametoa wito kwa walimu kuwafundisha wanafunzi sheria hiyo kupitia somo la uraia.
Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya Karatu ndugu. Abdala Nyange amesema katika taarifa yake, wamesikiliza mashauri 231 katika kipindi cha mwaka 2017/2018. Amesema wamesikiliza mashauri ya kimwili ya wanawake 100, jumla ya wanaume 30 wamefanyiwa ukatili wa kimwili, na ukatili wa kijinsia ni wanawake 106 na wanaume 46. Wanawake waliofanyiwa ukatili wa ngono ni 49 na waliolawitiwa ni 5 mashauri yote yamefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na huduma ya unasihi ikiwa ni pamoja na kuwapeleka Polisi na Mahakamani.
Ndugu. Abdala amesema watoto 87 wameondolewa mtaani katika kipindi cha mwaka 2017/218, watoto hao wameunganishwa na huduma za elimu na kuunganishwa na kituo cha Mwema. Mwaka 2018 matukio ya watoto wa kike waliotelekeza na wazazi ni 21 na watoto wa wakiume 14. Amesema jumla ya watoto 15 walipata makao mbadala kutoka kwa ndugu, na wengine 15 waliunganishwa na huduma za makao.
Ndugu. Abdala amesema idara ya ustawi wa jamii imeratibu huduma makao kwa watoto 410. Amesema Mabaraza 48 ya ulinzi wa mtoto na mwanake yameundwa katika vijiji 41; na Halmashauri mwaka 2018 imeendelea kushughulika dhidi ya maswala ya ukeketaji wanawake, amesema wanawake 331 walibainika kuwa wamekeketwa. Watoto wenye umri kati ya miaka 10 na 18 wameondolewa katika ajira hatarishi kata ya Mang’ola. Mwaka (2019) Watoto 49 kati yao wakike 27 na wakiume 22 waliondolewa kwenye ajira hatarishi. Watoto 18 walikuwa wamemaliza elimu ya msingi mwaka 2017/ 2018 na kati yao watoto 20 bado walikuwa shule, kati ya darasa la tatu na sita. Watoto wa sekondari 2 walikuwa wakitumikishwa ajira hatarishi; Jumla ya watoto 9, wakike 7 na wakiume 2 hawajawahi kwenda shule kabisa walikuwa wakifanya ajira hatarishi katika mashamba ya vitunguu.
Watoto wa kituo cha Mwema katika risala yao wamesema hali ngumu ya maisha ndani ya familia imekuwa ikisababisha watoto kukosa mahitaji muhimu, lakini pia wamesema kutengana kwa wazazi na kuowa au kuolewa na wenza wengine nayo kusababisha manyanyaso kwa watoto na kuwafanya kukimbilia mtaani.
Watoto wa kituo cha Mwema wamesema ulevi uliokithiri hufanya wazazi kusahau malezi hivyo kusababisha watoto kukimbilia mtaani. Wamesema athabu kali za nyumbani na shuleni husababisha pia watoto kukimbilia mtaani.
Watoto wa kituo cha Mwema wamesema adha wanazopata watoto wanaoishi mtaani ni pamoja na kutumikishwa kwa ngono. Kulala nje kwenye baraza au kulala kwenye mapagale na kuuza vyakula kwenye magenge. Wamesema athari nyingine ni pamoja kujiingiza kwenye tabia za wizi, kutumia madawa ya kulevya.
Watoto wakijiandaa katika kuazimisha siku ya mtoto wa mtaani duniani.
Watoto wakipita katikati ya mji,wakiadhimisha siku ya mtoto wa mtaani.
Watoto wakiwa katika Uwanja wa Mazingira Bora kuadhimisha siku ya mtoto wa mtaani.
Watoto wa kituo cha Mwema wakiwa wameshika bango lao katika madhimisho ya mtoto wa mtaani.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa