Kikao cha baraza la madiwani kimeendelea kwa siku ya pili mfululizo kwa kupata taarifa kutoka kamati za Halmashauri. Kikao hicho cha baraza kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Emmanuel Gege.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo ametoa maelekezo kwa baraza kufuatilia ukusanyaji wa mapato vizuri. Amesema amegundua kuna udanaganyifu unafanywa na watumishi wa serikali kwa kutumia fedha wanazotoza kodi kwa njia ya point of sales (POS) na kuzitumia fedha hizo kinyume na utaratibu. Mhe. Theresia amesema ameshampa maelekezo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu kufuatilia na kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji waliohusika. Amesema fedha za ukusanyaji wa mapato zinasaidia katika shughuli za maendeleo, kumalizia miradi viporo na kulipa madai ya watumishi.
Mhe. Theresia amesema kuna udhaifu pia wa kiutendaji katika kitengo cha manunuzi cha Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Amesema kitengo hicho hakifuati sheria za manunuzi, Mhe. Theresia amesema amebaini hayo baada ya kuunda tume kuchunguza ujenzi wa hospital ya wilaya. Katika taarifa yake kamati ilibaini kuna vifaa vilinunuliwa na havikufika eneo la ujenzi lakini vimeshalipiwa, amesema kuna dawa zimenunuliwa kuzidi mahitaji za kunyunyiza wadudu ili kuzuia uharibifu wa mchwa. Lakin kuna kokoto zilizozidi mahitaji, rola zimenunuliwa nyingi kuzidi mahitaji, ameliagiza baraza kupitia kamati ya fedha kutimiza wajibu wao kukagua miradi. Mhe Theresia amesema amekabidhi TAKUKURU wilaya karatu taarifa hiyo ya uchunguzi wa ujenzi wa hospitali kwa ajili kuchukua hatua zaidi za kisheria.
Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Emannuel Gege akiongoza kikao cha baraza la madiwani
Ndugu waziri Mourice Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Karatu, amesema watu wanazitumia fedha za mapato ambazo zinapaswa kuwekwa benk. Ndugu Mourice amesema tayari ameshakamata baadhi ya watu na kuwaweka ndani kutokana na kutumia fedha za makusanyo ya mapato ya serikali kinyume na utaratibu.
Ndugu Waziri Mourice amesema amemuandikia Mtunza Hazina kwa maandishi akimuelekeza umuhimu wa kusimamia ukusanyaji wa mapato vizuri na pia kusimamia matumizi mazuri ya fedha. Ndugu Mourice amesema Halmashauri iko mbioni kufunga mfumo wa mapato ofisi ya mkuu wa Wilaya ili kusaidia kuona mwenendo wa ukusanyaji wa kodi wa Halmashauri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa