Maadhimisho ya siku ya wauguzi yamefanyika katika tarafa ya Eyasi wilayani Karatu. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe.Theresia Mahongo ndiye aliyapokea maandamano ya wauguzi yaliyoanzia Madukani mbuga nyekundu nakuishia katika kituo cha afya Mbuga Nyekundu.
Mhe. Theresia alipata nafasi ya kuwafariji wagonjwa waliokuwa wakipata tiba katika kituo hicho cha afya Mbuga nyekundu. Tukio hilo lilifuatiwa na tukio la kula kiapo kwa wauguzi hao mbele ya mgeni rasmi. Wauguzi pia walitumia tukio hilo kuwaaga wenzao waliofikia umri wa kustaafu katika utumishi wa umma.
Mhe.Theresia amewapongeza wauguzi kwa kazi wanayofanya katika kutoa huduma kwa wananchi amewapa ari ya kufanya kazi kwa kujituma.Mhe. Theresia amesema hata kwenye risala mliyosoma neno lililotawala ni upendo katika kufanya kazi ya uguzi. Kuna mambo mengi mazuri mnayafanya lakini jambo moja tu likitokea watu wanaanza lawama, naomba msivunjike moyo. Kuna watu wamekuja kufanya uguzi kama kazi na siyo kama wito, hao ndio wanaowachafua katika utendaji wa kazi. Naombeni wauguzi mfanye kazi zenu kama mlivyo apa.
Mhe. Theresia amewapongeza wadau wote wa afya kwa kazi kubwa wanazofanya, ameomba shirika la world vision kumalizia kulifanyia ukarabati jengo la kituo cha afya Mbuga Nyekundu, ili jengo hilo lianze kutumika. Amesema anatambua mchango wa wadau wa afya wa sekta binafsi na umma katika kuboresha sekta ya afya.
Mhe. Theresia amewataka viongozi wa matawi wa vyama vya wafanyakazi kuwasemea wanachama kwenye ngazi ya taifa, juu ya malalamiko ya wauguzi kukatwa mshahara na vyama vya TUGHE na TALGWU badala ya chama chao cha wauguzi TANNA.
Mhe. Theresia amesema serikali imejikita katika ujenzi wa reli ya kisasa (standad Gauge) pamoja na mradi wa kufufua umeme wa stigler George. Ili umeme wa uhakika upatikane kuendeshea viwanda na matumizi ya manyumbani. Miradi hiyo inagharimu serikali fedha nyingi katika utekelezaji wake, ameomba wafanyakazi kuvuta subira. Amesema serikali inawajali sana wafanyakazi, na itatoa nyongeza ya mshahara nzuri. Mhe. Theresia amesema serikali bado inaendelea kuajiri wafanyakazi imeajiri walimu sasa na itaajiri pia watu wa kada ya afya.
Awali katika risala yao iliyosomwa na Bi,Suzan Henry Ngosi amesema muuguzi ni wakili wa mgonjwa kwa kumsemea haki zake. Muuguzi ni kiungo anayeunganisha kada zote za afya, muuguzi hupata lawama nyingi kwa mgonjwa au mteja anayekuwa katika huduma yanapotokea matokeo mabaya. Jitihada nyingi zimekuwa zikifanywa na wauguzi kwa wagonjwa; kama kutoa elimu ya kupambana na malaria kwa kinamama wajawazito, namna ya kupata hati punguzo na kupata dawa ya kuzuia malaria. Jitihada za kutoa kliniki ya mkoba katika maeneo ambayo hayana vituo vya kutolea huduma za afya. Wauguzi wameendelea na hamasa juu ya upimaji wa afya kwa hiari hosipitalini, kwenye mihadhara na kliniki.
Mkuu wa wilaya Mhe.Theresia Mahongo akimjulia hali mgonjwa katika kituo cha afya Mbuga nyekundu.
Wauguzi wakiwa wanafuatialia matukio katika sherehe ya siku ya wauguzi.
Wauguzi wakiwa katika ukumbi wa kituo cha afya Mbuga Nyekundu.
Wauguzi wakifuatilia kwa umakini matukio mbalimbali katika sherehe ya siku ya wauguzi.
Wauguzi wakiwa wameshika mishuma tayari kwa kula kiapo.
Wauguzi wakiwa wanajiandaa kula kiapo mbele ya mgeni rasmi.
Wauguzi wakinyoosha mikono wakati wa kuapa.
Wauguzi wakiwa katika kiapo wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa