Mama akiwa anafurahia mtoto wake katika sherehe ya siku ya mtoto wa Afrika
Maadhimisho yasiku ya mtoto wa Afrika ngazi ya wilaya yamefanyika katika Tarafa ya Endabash. Sherehe hizo zimeenda sambamba na uzinduzi wa chanjo ya vitamin A kwa watoto wadogo. Mgeni rasmi katika sherehe ya siku ya mtoto wa Afrika alikuwa mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo.
Mhe. Theresia amelipongeza shirika la World vision kwa ujenzi wa miundo mbinu yaa madarasa maji na afya. Mhe. Theresia amesema Way-Bantwana na Shidepa wametekeleza mradi wa waache wasome ambao unaenda vizuri na wameandaa vikundi vya kuinua uchumi wa wananchi vinavyoshirikisha wanawake na wakinababa wachache. Mhe. Theresia amewapongeza shirika la Compassion kwa kuwalipia ada na kuwaendeleza watoto katika mafunzo ya Tehama pia amewapongeza pia vituo vinane vya kulea watoto.
Mhe. Theresia Mahongo amewapongeza wadau kwa kupunguza tatizo la mimba shuleni. Amesema mwaka jana kulikuwa na mimba 15 shule ya msingi na sekondari 25. Mwaka huu kuna taarifa 2 za mimba kwa shule ya msingi na sekondari hakuna hili ni tatizo kubwa. Mhe. Theresia amesema swala la ajira za watoto limeendelea kuwa changamoto Tarafa ya Eyasi. Amewaomba wazazi kulionea haya jambo hilo imekuwa mtoto ndiye anayelea mzazi badala ya mzazi kumlea mtoto. Mhe. Theresia amemuagiza katibu Tarafa wa Eyasi kupambana na ajira za watoto katika mashamba ya vitungu kwa kuwakamata wazazi wanaojihusisha na kuwaachia watoto kwenda kufanya kazi kwenye mashamba ya vitunguu ili kujipatia ujira.
Mhe. Theresia amesema wazazi wamerudi nyuma katika kujitolea kuwapatia chakula watoto wanapokuwa shuleni. Amesema tarafa ya Endabash imerudi nyuma katika swala la kuwapatia watoto chakula shuleni. Amesema ni shule moja ya Raja inayotoa chakula cha mchana kwa watoto, amesema unapomnyima mtoto chakula unamsababishia udumavu. Mtoto anashindwa kufanya vizuri shuleni kutokana na kukosa chakula. Kuna sheria na 21 ya mtoto ya mwaka 2009 na kanuni za mtoto. Sheria hii inaonesha mzazi ambaye hamtunzi mtoto apewe adhabu zinazo muwajibisha. Amesema kauli mbiu inasema “mtoto ni msingi wa taifa endelevu, tumtunze, tumlinde na kumuendeleza” Mhe. Theresia amesema hata sita kumchukulia hatua mzazi yeyote ambaye anashindwa kumhudumia mtoto kwa kumpatia chakula anapokuwa shuleni. Amesema watoto wanavipaji mbalimbali, wazazi tunapaswa kulea watoto ili watimize ndoto zao.
Mhe. Theresia amewaasa wanachi kuhifadhi chakula amesema kuna maeneo kama ya kata ya Mbulumbulu na Mang’ola wamepata chakula. Amesema maeneo ya Endabash mpaka Baray Khusumay na kule Rhotia mazao hawakupata vizuri ni vyema kuhifadhi na kununua akiba ya chakula.
Mhe. Theresia amesema kuna uchaguzi wa serikali za mitaa, amewaomba wanachi kujitokeza kupiga kura. Amesema ni vyema wananchi wakajiepusha na vitendo vya rushwa nyakati za uchaguzi. Amesema ni vyema wananchi wakachagua viongozi bora, ambao watakuwa chachu ya maendeleo.
Mhe. Theresia ametoa taarifa kwa wananchi juu ya kuwepo kwa kikao cha wafanyabishara kitakachofanyika tarehe 20 mwezi huu. Ameomba wafanyabishara wote kujitokeza ili waweze kusema changamoto zao zinazowakabili katika shughuli zao za kibiashara. Kikao hicho kitajumuisha wafanyabishara kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Karatu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa