Shirika la kikristo la Compassion limefanya semina ya siku tatu juu ya namna kumlinda mtoto juu ya unyanyasaji. Semina hiyo iliyoisha jana katika kanisa la T.A.G Karatu imehusisha wadau wanaojihusisha na malezi ya watoto.
Ndugu Lameck Karanga Afisa Tarafa wa Karatu amefunga semina hiyo na amesema ni vyema semina za ufahamu wa namna ya kuwalinda watoto, wakapewa pia wazazi na jamii. Amesema semina kama hizo zinaweza zikafanywa shuleni, ambayo ni sehemu raisi ya kupata watoto. Amesema serikali itahamasisha kupitia mikutano ya umma ili wazazi na jamii iweze kupata ufahamu. Ndugu Lameck amesema kinga ni bora kuliko madhara yanayoweza kujitokeza baadae.
Bi, Elizabeth Madata, Afisa Ustawi wa jamii amesema semina hiyo imewasaidia kujifunza hatua za ukuaji wa mtoto. Maamuzi ya kuchukua pindi mtoto anapoathirika na unyanyasaji wa kijinsia lakini pia sehemu ya kuripoti pindi tattizo linapotokea. Bi Elizabeth amesema mtoto (infanty) anatakiwa awe karibu na wazazi wake hasa mama ili aweze ( Kujenga trust ) kuamini wazazi. Mzazi anatakiwa kumfutilia mtoto kwa karibu katika ukuaji wake ili aweze kujua kipaji chake.
Bi Elizabeth amesema changamoto walizokuwa wanazipata awali juu matukio ya unyanyasaji watoto ni mawasiliano duni kati ya wadau na vyombo vya serikali. Amesema kupitia semina hiyo imekutanisha wadau wote husika na imewasaidia kufahamiana lakini pia namna ya kuunganisha nguvu zao kwa pamoja dhidi ya unyanyasaji wa watoto. Amesema semina hiyo imewasaidia wadau kufahamu sehemu za kuripoti pindi matukio ya unyanyasaji yanapotokea. Amesema kuna hofu ya kutoa taarifa kwenye tukio la ukatili wa kijinsia kwa kuogopa uhasama, semina hiyo imewajengea uelewa mkubwa wadau.
Bw. Amani Lohay ambaye ni mdau amesema kwao katika semina hiyo, shirika la compassion limewapa njia nne za kuhudumia watoto amabazo ni kimwili kwa kumpa chakula na mazoezi. Lakini pia mtoto anajengwa kiroho kwa kupata mafundisho ya kiimani, na kiakili kwa mtoto kupewa akili ya ujasiriamali na ubunifu. Watoto wanajengewa namna njema ya kuhusiana na jamii na kuishi maisha yanayofaa.
Naye Mchungaji Samweli Kibola amesema mtoto wamekuwa wakinyanyaswa na kumekuwa hakuna mtetezi. Jamii imekuwa na mwamko duni wa kutetea haki za watoto, semina hiyo imesaidia mbinu za kumlinda mtoto. Amehimiza wazazi kutambua wajibu wao na kutimiza majukumu ya kumlinda mtoto
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa