Waziri wa ardhi nyumba maendeleo na makazi Mhe. William Lukuvi amefanya ziara wilayani Karatu leo, na kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa Mazingira Bora Karatu. Katika mkutano huo waziri wa ardhi aliongozana na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.
Katika mkutano wake Mhe. Lukuvi amesikiliza kero za ardhi za wanachi zaidi ya 250 zilizokuwa zimewakilishwa kwake kupitia kampeni yake mpya inayoitwa FUNGUKA KWA WAZIRI. Mhe. Lukuvi ametoa maagizo kwa watendaji kundesha zoezi la kukagua watu walio lipa kodi ya ardhi. Amesema watu binafsi, wenye mashamba makubwa, mashirika na vyama vya ushirika vyenye maeneo makubwa ya ardhi kuhakikisha wanalipa kodi ya ardhi vinginevyo watanyang’anywa.
Mhe. Lukuvi amewaonya watu wenye maeneo makubwa ya adhi kuyatumia kama walivyo omba na sio kukodisha kwa watu wa chini. Amesema atakayebainika kutumia ardhi kwa kukodisha masikini atafutiwa umiliki wa ardhi hiyo hata kama analipa kodi ya ardhi. Amesema kampeni ya nguvu ya kulipa kodi ya ardhi ifanyike nyumba kwa anyumba. Wananchi wote walipe kodi ya ardhi ispokuwa wale waliondolewa kulipa kodi ya ardhi.
Mhe. Lukuvi amesema asilimia tisini ya matatizo ya ardhi Karatu yanatokana na uvamizi wa maeneo ardhi wenyewe kwa wenyewe. Halmashauri wekeni bajeti ya matumizi bora ya ardhi kwenye viijiji ili kuondoa migogoro ya ardhi. Wananchi mlio vijijini pimeni ardhi ili muweze kupata hati za kimila kwa sababu zinakupa ulinzi madhubuti wa eneo lako. Wananchi wanaomiliki ardhi kwa hati za kimila hawatalipa kodi ya ardhi.
Mhe. Lukuvi ametatua mgogoro wa eneo la shule la Ganako na mzee Daniel, ameelekeza Mzee Daniel alipwe fidia na Halmashauri ili aondoke katika eneo hilo. Tunapofanya miradi ya maendeleo ya serikali kuna sheria zinazoruhusu kutwaa ardhi kwa manufaa ya umma. Amesema eneo la mzee Daniel lazima liwe ndani ya shule hivyo atalipwa kutokana na thamani ya ardhi na nyumba yake ili atoke katika eneo hilo.
Mhe. Lukuvi amesema kuna kesi ya kijiji cha Endala kati muwekezaji ndugu Mroso aliyechukua ardhi ya kijiji cha Endala na kuwa miliki yake. Amesema zoezi la kuhamisha ardhi ya kijiji kwenda kwa mtu binafsi halikwenda kwa utaratibu unaokubalika. Mhe. Lukuvi amemuelekeza Ndugu Mroso aliyetwaa ardhi hiyo kurudisha hati ya ardhi hiyo kesho kwa sababu haukufuata utaratibu mzuri.
Mhe Lukuvi amesema kuna makaburi mawili ambayo yapo kwenye Hotel ya Acacia yalizikwa wakati eneo lile likiwa kijiji sasa ni mji. Makaburi yale yanapaswa kuhamishwa na kuzikwa upya kwenye maeneo mengine ya makaburi kwa heshima. Mhe. Lukuvi amesema makaburi hayo yanapaswa kulipwa fidia, hivyo Halmashauri ya Karatu itoe notice kwa ajili ya zoezi hilo
Mhe..Lukuvi amesema kuna watu wamevamia eneo la Acacia na Tembotembo ambao ni watu maskini, amemuelekeza Mkuu wa Wilaya azungumze na wakurugenzi wa Acacia na Tembotembo ili watafute namna bora ya kuwabakiza wanachi hao waliovamia eneo hilo
Mhe.Lukuvi akipokea moja ya lalamiko kutoka kwa mwanachi
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa