Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amefanya mkutano na wananchi wa Karatu katika uwanja wa mazingira bora. Ametumia mkutano huo pia kusikiliza kero mbalimbali za wananchi wa wilaya ya Karatu walizo mueleza.
Mhe. Theresia amesema Karatu mjini kuna vibaka sana jambo linalo hatarisha usalama wa wananchi na mali zao. Amesema vibaka hao wengi ni vijana, amesema kama inafikia mahali huwezi ukaweka nguo nje zimepitiwa huwezi ukafuga kuku watu wameiba inaumiza sana. Amesema Karatu tunategemea utalii sana, kuna watu wanapita kwenda mbugani ndio maana tunafanya biashara. Amesema hatuwezi kuwa na taifa la wezi na vibaka, amekumbusha na kusisitiza wafanya biashara kufunga kamera za ulinzi kwenye biashara. Ameelekeza wenyeviti wa vitongoji kuanza ulinzi shirikishi ili kukabiliana na uhalifu wa wizi unaoendelea na kuhatarisha hali ya usalama wa watu na mali zao.
Mhe. Theresia amesema kama Mkuu wa wilaya jukumu lake ni kusimamia ulinzi masaa 24, amewaasa wananchi juu ya kupanda mshikaki.amesema kwenye mtandao kuna matukio mengi ya watu kuvamiwa na kunyang’anywa pikipiki zao hasa nyakati za usiku. Amewaasa wananchi kuchukua tahadhari hasa nyakati za usiku kwa kupanda pikipiki kwa mtu unayemfahamu.
Amezungumzia pia swala la madereva bodaboda, amesema kwenye kikao walichokaa waendesha bodaboda walikubaliana muda wa mwisho wa kufanya kazi ni saa sita usiku. Amesema kuna vituo viwili ambavyo vina leseni ya kufanya biashara usiku kucha, hapo bodaboda walikubalina katika vituo hivyo viwili kuwepo na kufanya shughuli zao. Hivyo hata wakikutwa na watu wa ulinzi shirikishi watajitambulisha na wataendelea na kazi zao.
Wananchi wakifuatilia mkutano katika uwanja wa mazingira Bora
Mhe. Theresia amesema muda wa mwisho wa kufunga baa kwa siku za kazi ni saa tano usiku na hufunguliwa saa kumi alasiri baada ya mida ya kazi. Amesema kwa siku za sikukuu au mwishoni mwa juma baa hufunguliwa saa kumi na kufungwa saa sita usiku.
Mhe. Theresia amewaasa wananchi kuacha mila potofu za kuficha uovu, amesema watu wanao fanya uovu wanafahamika. Nivyema wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi, ili wakamatwe na hatua kali dhidi yao zichukuliwe. Kumekuwa na tabia za wananchi kuficha wahalifu hasa kwa wale watu wanaobaka mabinti. Amesema tabia hizi zinakatisha ndoto za wasichana kufikia malengo yao. Amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kubaini wahalifu na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Haiwezekani watu wafanye uhalifu halafu wanakubaliana kusuluhisha kwa kupeana madume ya ng’ombe.
Awali wananchi katika kikao hicho walimueleza mkuu wa wilaya kero zinazowasumbua, ndugu Onesmo Tarimo amemueleza mkuu wa wilaya kwamba kuna kesi za ubakaji nyingi ambazo jamii inazifumbia macho. Hakuna hatua za kisheria zinazochukuliwa juu yao baada ya wananchi kushindwa kutoa ushirikiano kwa polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe juu yao.
Naye Mwenyekiti wa kitongoji cha Bwawani Ndugu Joshua Nangay amemueleza kero wanazopata juu ya utofauti wa muda kufunga baa. Amesema kuna baadhi ya baa ni mali ya wafanyakazi na ni marafiki na jeshi la polisi, baa zao hazifungwi ila hizi za watu wengine zinafungwa mapema. Wezi na vibaka hukaa kwenye baa hizo wakati wakivizia kufanya uhalifu usiku, hivyo kumuomba mkuu wa wilaya kutoa maelekezo juu ya jambo hilo.
wanachi wakifuatilia mkutano kwa makini
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa