NA TEGEMEO KASTUS
Ziara za mkuu wa wilaya ya Karatu kutembelea ujenzi wa miundo mbinu ya elimu na afya inayoendelea katika maeneo mbalimbali imeanza kuleta matokeo chanya. Baada ya mradi wa afya Sumawe uliokuwa umetelekezwa kwa kipindi cha miaka tisa kukamilika.
Hayo yamebainika wakati wa ziara ya Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipotembelea zahanati ya Sumawe Mjini Karatu ambayo awali ujenzi wake ulikuwa umesimama. Mh.Kayanda ametoa maelekezo kwa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo kuhamisha nguvu katika ujenzi wa choo ili zahanati iweze kukamilika na kuanza kufanya kazi. Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya alitembelea kituo cha afya Endabash kukagua maendeleo ya ujenzi wa Maabara ambayo imefikia hatua ya kuweka kenchi. Ujenzi huo unajengwa kwa mapato ya ndani ya Halmashauri na ujenzi wa maabara ukikamilika utasaidia kituo hicho cha afya kuanza kutoa huduma ya upasuaji.
Muonekano wa zamani wa jengo la zahanati ya Sumawe
Muonekano wa sasa wa zahanati ya Sumawe
Wakati huo huo Mh. Kayanda amtembelea ujenzi wa madarasa matatu sekondari ya Florian na ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya sekondari ya Qaru pamoja na choo. Ujenzi huo unatarajia kufikia katika hatua ya lenta ifikapo jumamosi. Katika shule ya Msingi Bwawani Mh. Kayanda amekagua hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa madarasa matatu pamoja na eneo ambalo linatarajiwa kujengwa choo na S/M Gyekrum amekagua ujenzi wa madarasa mawili fedha zote zimetolewa na serikali kupitia EP4R.
Mh.kayanda amehimiza wakandarasi kuzingatia muda wa ukomo wa kumaliza miradi uliowekwa na serikali lakini pia kuhakikisha ujenzi wa majengo unaendana na thamani ya fedha zilizotolewa ikiwa ni pamoja na kuweka madawati.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa